Idara ya Fedha na Biashara katika Halmashauri Manispaa ya Kinondoni inasimamia masuala yote yanayohusiana na Fedha na Biashara katika utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri. Idara ina Ofisi za Mapato, Matumizi, Mishahara, Sehemu ya Ufungaji wa Mahesabu na Biashara.
Kitengo cha Biashara ni Kitengo kilichopo chini ya Idara ya fedha na Biashara. Kitengo hiki kinalojukumu kubwa la kutoa leseni za biashara pamoja na leseni za vileo. Utoaji wa leseni hizi ni kwa mujibu wa Sheria kama ifuatavyo:-
Leseni za biashara zinatolewa chini ya Sheria ya leseni ya biashara Na. 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake ya 1980, 2013 kifungu 11(1) na marekebisho ya mwaka 2015.
Leseni za vileo zinatolewa chini ya Sheria ya vileo ya mwaka 1968 kifungu Na. 28 na marekebisho yake ya mwaka 1981 na 2011.
Ushuru wa makazi unatozwa kwa kutumia sheria ya ulipaji wa Huduma za jiji Na. 23 (1972).
Kitengo cha Biashara pia kinayo majukumu mengine ambayo kinayatekeleza kama ifuatavyo;-
Leseni zote za biashara hutolewa kwa kujaza fomu ya maombi Na. TFN – 211. Mwombaji anatakiwa awe na umri wa miaka 18 au zaidi. Fomu yake ya maombi inatakiwa iambatishwe na nyaraka zifuatazo:-
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255 22 2170173
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.