KITENGO CHA MANUNUZI NA UGAVI
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ina kitengo cha Manunuzi na ugavi kinachoundwa kwa mujibu wa sheria ya Manunuzi Na 7 ya mwaka 2011 kifungu na 37 na Kanuni namba 446 za mwaka 2013 ambapo sheria hiyo inaitaka taasisi ya serikali iwe na Kitengo kinachosimamia usimamizi wa manunuzi (Procurement Management Unit –PMU).
Kwa Manispaa ya Kinondoni, Kitengo cha Ugavi kina wataalamu 14 ambao wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ya manunuzi na kinalo jukumu kubwa la kusimamia manunuzi yote toka idara na vitengo vilivyoko kwenye Halmashauri.
• Kuhakikisha Sheria na Kanuni za Manunuzi zinazingatiwa.
• Kuhakikisha huduma na bidhaa zinapatikana kwa wakati ili Halmashauri iweze kutekeleza majukumu mengine yanayohitjika na jamii.
• Kuhakisha bidhaa , kazi za Ujenzi na huduma zote zinalingana na thamani halisi ya Fedha
• Kuwepo na uwazi katika fursa mbalimbali za zabuni.
• Kuwepo na usawa katika kutoa zabuni mbalimbali.
Majukumu ya kitengo cha ugavi yameainishwa kwenye sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kipengele Na 38 kama yalivyo ainishwa hapa chini:-
• Kushughulikia manunuzi yote ya taasisi
• Kusaidia majukumu ya Bodi ya Zabuni
• Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni
• Ni sekretarieti ya Bodi ya Zabuni
• Kuandaa na kupitia orodha ya mahitaji
• Kuandaa nyaraka za Zabuni
• Kuandaa matangazo ya Zabuni
• Kuandaa mikataba
• Kutoa mikataba iliyokwisha kusainiwa
• Kutunza kumbukumbu za manunuzi
• Kutunza orodha au rejesta ya kikataba yote iliyoingiwa
• Kuandaa taarifa ya mwezi ya Bodi ya Zabuni.
• Kuandaa mpango wa mahitaji
Aidha Kitengo cha Ugavi mbali na kufanya kazi na Idara na Vitengo vya Halmashauri, pia kinafanya kazi kwa karibu sana kwa kushirikiana na Bodi ya Zabuni ya Halmashauri ambayo majukumu yake yameainishwa na sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kifungu cha 33 (1) (a) –( e).
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255 22 2170173
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.