Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji inashughulikia upangaji na uratibu wa mipango ya maendeleo ya Halmashauri, usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ya Halmashauri, ukusanyaji wa takwimu pamoja na kuratibu shughuli za uwekezaji. Idara hii imegawanyika katika sehemu tatu kama ifuatavyo:-
1. Sera na Mipango
2. Usimamizi na Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo
3. Takwimu
Majukumu ya sehemu hii ni kama ifuatavyo:-
• Kuratibu uandaaji wa Mipango shirikishi katika Kata zote za Halmashauri kupitia Mfumo wa O&OD kila mwaka
• Kuratibu na kuandaa Mpango na Bajeti ya kila mwaka ya Halmashauri
• Kuratibu uandaaji wa maandiko ya miradi mbalimbali ya maendeleo (Project Proposal)
• Kusimamia uandaaji wa mpango wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kila mwaka
• Kusimamia uandaaji wa mpango kazi (Action Plans) ya bajeti kila mwaka
• Kuratibu maandalizi ya Sera na Mpango Mkakati wa Halmashauri.
Majukumu ya sehemu hii yapo kama ifuatavyo:-
• Kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo
• Kuandaa taarifa za Miradi ya maendeleo ya Halmashauri kila robo mwaka
• Kuandaa mapitio ya bajeti ya kila mwaka baada ya kipindi cha nusu mwaka
Sehemu hii hushughulikia masuala yanayohusu takwimu mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kuratibu shughuli za utafiti kama ifuatavyo:-
• Kuratibu na kusimamia benki ya takwimu ya Halmashauri.
• Kuhuisha na kuboresha takwimu za Kiuchumi na Kijamii (Social-economic Profile) ya Halmashauri
• Kuratibu na kuhifadhi takwimu za Idadi ya watu za Halmashauri kwa kutumia rejista za wakazi wa Mitaa.
• Kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango mkakati wa Halmashauri.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255 22 2170173
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.