• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Matukio ya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo cha mijini
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji, mifugo na uvuvi
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Baraza la Madiwani
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Umma
  • Mifumo
    • NaPA
    • eMrejesho

ZAIDI YA NYUMBA 100 ZIMEBOMOKA NA NYINGINE 700 KUZUNGUKWA NA MAJI WILAYA YA KINONDONI.

Tarehe iliyowekwa: October 30th, 2017

 NI KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA NA KUSABABISHA ATHARI KUBWA IKIWEMO WATU WAWILI KUPOTEZA MAISHA. 

 Watu wawili Wilaya ya Kinondoni wanasadikiwa kupoteza maisha kufuatia mvua kubwa zinazoendele kunyesha katika jiji la Dar es salaam 

 Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi alipofanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo kwa lengo la kujionea hali halisi ya athari zilizosababishwa na mvua.

 "Leo kama mnavyofahamu kumekuwepo na mvua ambazo zimeleta madhara makubwa katika Wilaya yetu ya Kinondoni, ziko taarifa ambazo zimethibitisha mpaka sasa tunao wananchi wawili ambao wamepoteza maisha kutokana na mvua ambazo zinaendelea, tunaendelea kukusanya taarifa kutoka maeneo mengine kupitia jeshi la polisi lakini mpaka sasa idadi iliyothibitika ni wawili," Amebainisha Hapi 

 Amesema takribani nyumba mia moja zimebomoka kufuatia mvua hizo na nyingine  mia saba kuzungukwa na maji kitu ambacho kimeleta  athari  kwa wananchi waliowengi katika maeneo hayo.

 "Tunazo nyumba ambazo ni zaidi ya mia saba ambazo zinakadiriwa zimezungukwa na maji lakini kadhalika tunazo nyumba zaidi ya  mia moja ambazo zinasadikika zimebomoka katika kata zetu zote na katika mitaa mbalimbali ya Wilaya ya Kinondoni, mvua ambazo zimenyesha zimeleta madhara makubwa sana "Amesema Hapi .

 Aidha amewataka Maafisa Mipangomiji wa Manispaa kuhakikisha wanafuatilia uhalali wa maeneo hayo kwa ramani za Mipangomiji na kujiridhisha kama maeneo hayo yaliyoathirika yalitengwa kwa ajili ya makazi ya watu. 

 "Maafisa Mipangomiji, angalieni uhalali wa maeneo haya, yalitengwa kwa matumizi gani "Alisisitiza Hapi 

 Ameongeza kuwa kwa mujibu wa sheria, Mwananchi yeyote anapaswa kujenga umbali wa mita 60 kutoka  chanzo cha mto.

 Katika hatua nyingine amewataka wananchi waliojenga maeneo hatarishi kuhakikisha wanachukua tahadhari ili kuepukana na madhara yanayoweza kutokea kufutia mvua hizi zinazoendelea kunyesha. 

 "Wako baadhi ya wananchi wetu ambao wamejenga katika meneo yasiyoruhusiwa kisheria, kule mbezi kunawanchi wamejenga kandokando ya mto na sheria yetu inasema mita 60 kutoka chanzo cha mto haparuhusiwi kujengwa nyumba yeyote, wako baadhi ya wananchi wamejenga kwenye mabonde, maeneo ya mkondo wa maji maeneo ya mabonde na mabwawa hawa ndio wananchi ambao wamekuwa wahanga wakubwa sana wa mvua hizi ambazo zinaendelea kwa hiyo nitoe wito tu kwa wanachi wote ambao wako katika meneo hatarishi, waondoke haraka kupisha yanayoweza kujitokeza, wenzetu wa hali ya hewa wanasema mvua hizi zinaweza kuendelea na zinaweza kushika kasi zaidi ya hapa tuliposhuhudia"Amesisitiza Hapi. 

 Ametoa wito kwa wananchi kuvuta subira wakati Serikali inajipanga kutatua changamoto zilizotokana na mvua hizo na mamlaka husika kupiga dawa kwenye mabwawa, na madimbwi ikiwa ni pamoja na kusafisha mitaro kama hatua za awali za kujilinda dhidi ya mgonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu. 

 Maeneo aliyoyatembelea Mkuu huyo wa wilaya ni Boko basihaya lililopo kata ya Bunju, Mto Nyakasangwe, Mto Mpiji ulioko Kata ya Mbweni, Daraja la Mbezi, eneo la Msisiri b,  lililoko Kata ya Mwananyamala. 

 Imetolewa na
 Kitengo cha Uhusiano
 Manispaa ya Kinondoni

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 13, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA DEREVA DARAJA II September 21, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI (TAREHE 20 SEPTEMBA, 2021) September 21, 2021
  • TANGAZO LA KUWAPANGA WAFANYABISHARA KATIKA MAENEO RASMI September 28, 2021
  • Tazama zote

Habari mpya

  • BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU KINONDONI LAFANYIKA LEO

    May 18, 2022
  • KINONDONI KUFIKIA WATOTO TAKRIBANI 156871 KAMPENI YA SIKU NNE CHANJO YA POLIO KITAIFA

    May 18, 2022
  • MWENGE WA UHURU KINONDONI 2022, WAPITIA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI TAKRIBANI BILIONI 3.9 FEDHA ZA KITANZANIA

    May 10, 2022
  • MEYA KINONDONI AFUTURISHA

    April 27, 2022
  • Tazama zote

Picha Jongefu

POSHO MADIWANI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.