• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Matukio ya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo cha mijini
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji, mifugo na uvuvi
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Baraza la Madiwani
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

WATAALAMU WA LISHE TAFUTENI LUGHA RAHISI YA KUFIKISHA UJUMBE KWA JAMII

Tarehe iliyowekwa: February 9th, 2022

Ni agizo lake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kawe katika maadhimisho ya siku ya lishe yaliyofanyika katika viwanja ya Tanganyika Pakers leo.

Amesema jamii ndio msingi imara wa maendeleo hivyo nguvu nyingi ielekezwe kwao kwa kutoa elimu rahisi ya lishe itakayowapelekea kuwa na uelewa wa pamoja kuhusiana na umuhimu wa mlo kamili na lishe kwa afya zao.

"Wataalam tafuteni lugha rahisi ya kutoa elimu kwa watu wetu kuhusiana na lishe, hii ni muhimu sana, kwani itawasaidia kuhakikisha wanapata  mlo kamili kwenye vyakula vyao, ikiwezekana tumieni majina ya rangi kwani ndio mazingira wanayoishi kwenye jamii". Amesema Mhe. Gondwe.

Aidha amesisitiza pia umuhimu wa lishe kwa wanawake wajawazito ndani ya siku mia moja tangu kupata ujauzito na siku 1,000 baada ya kujifungua, ikiwemo chanjo muhimu na kuwataka waalimu kuwasisitiza wazazi kuwa na mpango mkakati wa lishe kwa watoto wao hali itakayowaondolea udumavu uliosababishwa na kukosa  mlo kamili au mlo ulio bora.

Naye Mkuu wa Idara ya Mifugo Bi. Betila Lyimo, alipotakiwa kuzungumza amesema lishe inayotokana na mifugo ni lishe imara iliyo na virutubisho muhimu mwilini inayompasa mwanadamu yeyote kutumia  na kuahidi kufanyika kazi maelekezo yote hususan utoaji wa elimu ya lishe kwa jamii kwa kutumia njia iliyo rahisi ili wote kwa pamoja tuweze kuwa  na afya bora ili tusukume gurudumu la maendeleo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wajasiriamali kuhakikisha wanakuwa wabunifu na  kuzitangaza bidhaa zao kwa kuzipa majina, rangi na nembo itakayotoa utambulisho.

Maadhimisho hayo ya lishe pia yamehudhuriwa na wadau wa lishe, viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali,  Watendaji wa Kata na Mitaa, wananchi, Idara ya mifugo, wajasiriamali  pamoja na wanafunzi kutoka shule ya Msingi Tumaini.

Imeandaliwa na

Kitengo Cha Habari na Uhusiano.

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI KWA VITENDO (PRACTICAL) June 30, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KWA NAFASI YA DEREVA DARAJA II June 29, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO ULIOFANYIKA TAREHE 28 JUNI, 2022 June 28, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 20, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • UHUSIANO WA DSM NA HAMBURG WAFANIKISHA UZINDUZI KIWANDA CHA MBOJI

    June 30, 2022
  • VIKUNDI 286 VYA WANUFAIKA WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 VYAPATIWA MAFUNZO

    June 20, 2022
  • MAFUNZO KAZI YA MFUMO WA UTOAJI, USIMAMIZI WA MIKOPO YA ASILIMIA 10

    June 18, 2022
  • KINONDONI YAPONGEZWA KWA UJENZI WA KIWANJA CHA MICHEZO

    May 26, 2022
  • Tazama zote

Picha Jongefu

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.