• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Matukio ya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo cha mijini
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji, mifugo na uvuvi
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Baraza la Madiwani
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Umma
  • Mifumo
    • NaPA
    • eMrejesho

VIGEZO 14 VYA UPIMAJI VYAIPATIA KINONDONI TSH BILIONI 9, UJENZI WA SOKO -MAGOMENI

Tarehe iliyowekwa: May 8th, 2018

Vigezo 14 vilivyotumika katika mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza miradi yenye kuchochea Mapato, vyaipatia Kinondoni jumla ya tsh bil 9, kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa Magomeni.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Suleiman Jafo, katika hafla ya uzinduzi wa uwekaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika mamlaka za Serikali za Mitaa iliyofanyika katika ukumbi wa Treasure square Mkoani Dodoma.

Amesema mingoni mwa Halmashauri 17, kati ya 185, zilizoshindanishwa, Kinondoni imeibuka kidedea na kufikia vigezo vya kupatiwa fedha hizo, na kuwataka Mkurugenzi wake Ndg Aron Kagurumjuli, pamoja na Meya wake Mh Benjamin Sitta kuhakikisha wanasimamia fedha hizo kwa lengo lililokusudiwa.

Akiainisha vigezo hivyo vilivyotumika, Mh Jafo amesema lengo ni kuziwezesha mamlaka za Serikali za Mitaa, kujisimamia wenyewe Katika kutekeleza mpango mkakati wa miradi hiyo itakayoongeza Pato la Halmashauri.

Amevitaja vigezo hivyo kuwa ni andiko la mradi, upembuzi yakinifu, mtiririko wa fedha, uwezo wa kuongeza mapato, uwezo wa Halmashauri kusimamia mradi, uthibitisho wa umiliki wa ardhi, pamoja na uchambuzi wa viashiria vya uhimilivu.

Nyingine ni uwezo na mpango wa Halmashauri kujitegemea, michoro na usanifu, mpango wa matumizi ya eneo la mradi, hati safi ya ukaguzi wa hesabu, mpango mkakati wa Halmashauri, nyaraka za mradi na vielelezo kuchambuliwa na sekretarieti ya Mkoa husika, pamoja na uchambuzi ulioidhinishwa na OR-TAMISEMI.

Hafla hiyo ya utiaji saini imehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. A. Kijaji, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya, Wah. Wabunge, pamoja na Wakuu wa Mikoa.


Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari na Uhusiano.

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 13, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA DEREVA DARAJA II September 21, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI (TAREHE 20 SEPTEMBA, 2021) September 21, 2021
  • TANGAZO LA KUWAPANGA WAFANYABISHARA KATIKA MAENEO RASMI September 28, 2021
  • Tazama zote

Habari mpya

  • BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU KINONDONI LAFANYIKA LEO

    May 18, 2022
  • KINONDONI KUFIKIA WATOTO TAKRIBANI 156871 KAMPENI YA SIKU NNE CHANJO YA POLIO KITAIFA

    May 18, 2022
  • MWENGE WA UHURU KINONDONI 2022, WAPITIA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI TAKRIBANI BILIONI 3.9 FEDHA ZA KITANZANIA

    May 10, 2022
  • MEYA KINONDONI AFUTURISHA

    April 27, 2022
  • Tazama zote

Picha Jongefu

POSHO MADIWANI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.