• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Matukio ya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo cha mijini
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji, mifugo na uvuvi
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Baraza la Madiwani
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

TAMISEMI YAENDESHA MAFUNZO YA SIKU MOJA KWA KAMATI YA LISHE KINONDONI

Tarehe iliyowekwa: November 16th, 2018

 NI KUHUSIANA NA UANDAAJI WA MIPANGO YA HUDUMA ZA LISHE KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020.

 Ofisi ya Raisi -TAMISEMI kupitia kitengo cha lishe imeendesha mafunzo kwa Kamati ya lishe ya Manispaa ya Kinondoni, yahusuyo mipango ya utekelezaji wa  huduma za lishe kwa watoto umri chini ya miaka mitano, ikiwa ni pamoja na kuongeza uelewa katika swala zima la utekelezaji wake, hasa uwekaji wa vipaumbele katika bajeti ya 2019/2020.

 Akifungua mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo,  Bi Stella Msofe amesema mafunzo haya ni muhimu, na yakawe chachu ya utekelezaji wa jambo hili, hasa ikizingatiwa azma ya Serikali ni kuhakikisha inaepukana na madhara yanayoweza kutokea kwa watoto wetu pindi wanakosa lishe bora

 Naye mkufunzi kutoka ofisi ya Rais -TAMISEMI Bi.Mary Kibona, alipokuwa akiwasilisha mada  ihusianayo na mpango mkakati wa utekelezaji,amefafanua maana halisi ya  lishe kuwa ni  mchakato wa tangu chakula kinapoliwa mdomoni, kinasagwa na kuingia mwilini na kuanisha madhara ayapatayo mtoto anapokosa lishe bora kuwa ni  kupata upungufu wa madini na Vitamini mwilini.

 Akiainisha mafanikio ya Kamati ya lishe kwa Manispaa ya kinondoni tangu kuundwa kwake, Afisa lishe wa Manispaa hiyo Bi Emiliana Sumaye amesema , kamati hiyo imefanikiwa kupeleka shughuli za lishe kwa idara mtambuka, imefanikiwa kukaa vikao vitatu vya kujadiliana mwelekeo mzima wa lishe na kuainisha njia sahihi za kuhakikisha lengo linafikiwa, imefanikiwa pia kuhakikisha vituo 65 vya kutolea huduma za afya vilivyoko Manispaa vinatoa elimu ya lishe, na kufikia wazazi takribani 19,399 kwa elimu hiyo ya lishe kwa watoto na wajawazito.

 Pia ameainisha changamoto zinazowakabili kuwa ni Jamii kushindwa kutumia huduma ya uzazi kikamilifu, watoa huduma kutowajibika ipasavyo, kuwepo na  upungufu wa watoa huduma ngazi ya jamii, na watoa huduma kutopata elimu ya utoaji wa vidonge vya folic Acidi.

 Mafunzo haya yaliyohudhuriwa  pia na wawakilishi kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dar es salaam Bi Janeth Mzava, Mwakilishi kutoka, UNICEF Bi.Joyce Ndeba, Mwenyekiti wa huduma za Uchumi Afya na Elimu Mh.Thadei Masawe, kamati ya lishe ya Manispaa,  pamoja na wakuu wa idara na vitengo, yamejadili mada zihusuzo uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli za lishe.

 Nyingine ni Mpango na bajeti ya lishe kwa kutumia planrep, shughuli za lishe/afua za lishe zinazoweza kupangwa ngazi ya vituo vya afya na upatikanaji wa rasilimali watu na fedha.

 Imeandaliwa na,
 Kitengo cha Habari na Uhusiano.
 Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KWA NAFASI YA DEREVA DARAJA II June 29, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO ULIOFANYIKA TAREHE 28 JUNI, 2022 June 28, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 13, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIKUNDI 286 VYA WANUFAIKA WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 VYAPATIWA MAFUNZO

    June 20, 2022
  • MAFUNZO KAZI YA MFUMO WA UTOAJI, USIMAMIZI WA MIKOPO YA ASILIMIA 10

    June 18, 2022
  • KINONDONI YAPONGEZWA KWA UJENZI WA KIWANJA CHA MICHEZO

    May 26, 2022
  • BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU KINONDONI LAFANYIKA LEO

    May 18, 2022
  • Tazama zote

Picha Jongefu

POSHO MADIWANI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.