• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Matukio ya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo cha mijini
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji, mifugo na uvuvi
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Baraza la Madiwani
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

KINONDONI YAZINDUA RASMI ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI

Tarehe iliyowekwa: February 21st, 2022

Akizindua zoezi hilo kwa majimbo yake mawili ya uchaguzi, Mkuu wa Wilaya ya hiyo Mhe. Godwin Gondwe amesema uzinduzi huu ni katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan la kutaka utambuzi na uainishaji wa maeneo kwa majina na namba, hali itakayoleta tija kwa Taifa letu.

Amesema "Tumewatengenezea wananchi mfumo wa kuweza kuwafungulia uchumi wa kidigitali, kwa sababu sasa hivi kama mtu anafanya biashara yake mtandaoni, anaweza akapiga picha na kusema kuwa biashara yake iko wapi, lakini pia inamsaidia katika masuala ya usalama" Amesema Gondwe.

Ameongeza kuwa anwani za makazi pia ni maandalizi ya kuelekea kwenye sensa inayotarajiwa kufanyika tarehe 22 mwezi Agosti, mwaka huu, hali itakayorahisisha katika kufanikisha kwake .

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Songoro Mnyonge katika kuunga mkono azma ya uwekaji wa anwani za makazi kwa wananchi wake amesema jambo hili linapaswa kutekelezwa kwa ufanisi na umakini ili liweze kufikiwa lengo lililokusudiwa.

 Akitoa ufafanuzi wa hatua za awali ambazo Kinondoni imechukua mpaka sasa katika kufanikisha zoezi hili la anwani za makazi Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Hanifa Suleiman amesema Manispaa ya Kinondoni imeshakamilisha andiko pamoja na masuala ya bajeti ambayo ndio msingi mzima wa utekelezaji na ukamilishwaji wa jambo hili na kuwataka wana Kinondoni wote kutoa ushirikiano ili likamilike kwa wakati.

Uzinduzi huo pia umehudhuriwa  na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe  Kheri Misinga, Watendaji wa Kata na Mitaa, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wote pamoja na wananchi.



Imeandaliwa na

Kitengo Cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni.


Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI KWA VITENDO (PRACTICAL) June 30, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KWA NAFASI YA DEREVA DARAJA II June 29, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO ULIOFANYIKA TAREHE 28 JUNI, 2022 June 28, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 20, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • UHUSIANO WA DSM NA HAMBURG WAFANIKISHA UZINDUZI KIWANDA CHA MBOJI

    June 30, 2022
  • VIKUNDI 286 VYA WANUFAIKA WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 VYAPATIWA MAFUNZO

    June 20, 2022
  • MAFUNZO KAZI YA MFUMO WA UTOAJI, USIMAMIZI WA MIKOPO YA ASILIMIA 10

    June 18, 2022
  • KINONDONI YAPONGEZWA KWA UJENZI WA KIWANJA CHA MICHEZO

    May 26, 2022
  • Tazama zote

Picha Jongefu

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.