• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fukwe na Visiwa
    • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Matukio ya Utalii
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Iliyopangwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio

KINONDONI YAZINDUA MAONESHO YA BIDHAA ZA NGOZI VIWANJA VYA TANGANYIKA PACKERS, YAWEKA MKAKATI WA SOKO LA UHAKIKA

Tarehe iliyowekwa: December 12th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa katika kutatua changamoto ya kupata soko la uhakika la bidhaa za ngozi, Wilaya hiyo imejipanga kuwatafutia maeneo wazalishaji wa ndani ambapo wote watakaa sehemu moja kwa ajili ya uzalishaji na uuzaji wa bidhaa hizo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za ngozi yanayofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers , Mhe. Chongolo amesema kuwa mkakati huo utasaidia kuinua uhakika wa soko kwa wazalishaji.

Amefafanua kuwa maonesho hayo ya bidhaa za ngozi yanafanyika kwa mara ya kwanza katika Wilaya hiyo na kwamba ni lazima kila mwananchi ajenge utamaduni wa kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kuwataka kuondokana na dhana ya kuona bidhaa zinazotoka nje ndio bora zaidi.

“ Ukienda kwenye nchi za wenzetu hasa zilizoendelea, wao wanathamini kwanza cha kwao, cha mwingine badae, nasisi tukifikia hatua hiyo tutafanikiwa sana, lakini tutafikaje hapo ni la zima kuanzia sasa tuamke tuanze kupenda vya kwetu” amesema Mhe. Chongolo.

Mhe. Chongolo ameongeza kuwa uwepo wa maonesho hayo utaongeza tija na mipango madhubuti ya kuhakikisha kuwa mpango huo unakuwa endelevu sambamba na kuongeza wigo mpana wa kutangaza bidhaa hizo na wananchi kupenda kuzitumia.

“ Uwepo wenu hapa utawezesha wale wananchi ambao wanakuja kununua bidhaa zenu , ndio watakuwa mawakala kwa wananchi wengine ambapo na wao watapenda kuja kununua bidhaa hizi bora na nzuri za kitanzania” ameongeza.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kawe , Mhe. Muta Rwakatare amempongeza Mhe. Chongolo kwa kubuni na kufanikisha kuwepo kwa maonesho hayo.

Ameongeza kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao mkuu huyo wa Wilaya wa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi, anaamini kuwa sasa ni wakati wa wajasiriamali hao kunufaika kwani changamoto zao pia zimefikia kikomo.

Ameongeza kuwa Rais Dk. John Magufuli amekuwa mstari wa mbele kusisitiza uchumi wa viwanda na kwamba hadi sasa tayari adhma hiyo imefanikiwa kwa asilimia kubwa.

Naye Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Patricia Henjewele amesema kuwa wazo la kuwepo kwa maonesho hayo lilitolewa na Mhe. Chongolo wakati wa maonesho ya nanenane ambapo alihitaji kuandaliwa kwa mpango kazi wa kuwa na maonesho hayo.

Amesema kuwa kabla ya kufanyika kwa maonesho hayo, awali yalifanyika mafunzo ya siku nne ambayo yaliendana sambamba na maonesho ya bidhaa hizo kwa siku moja yaliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Maonesho hayo ya siku nne yatafikia kilele Disemba 15 ambapo bidhaa zote za ngozi ikiwemo viatu, mikoba, mikanda na mabegi ya shule ya wanafunzi yanapatikana hapo.

Imetolewa na

Kitengo cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni

Matangazo

  • TANGAZO KUHUSU WAFUGAJI WENYE MIFUGO INAYOZURURA OVYO January 30, 2023
  • TANGAZO ULIPAJI WA TOZO January 26, 2023
  • TANGAZO KWA WAOMBAJI WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA MAPATO YA NDANI November 24, 2022
  • MABADILIKO YA SIKU YA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WA MAUDHUI, WASIMAMIZI WA TEHAMA NA MAKARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 July 28, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • PUNGUZENI MATUMIZI YA KARATASI-NDUMBARO

    February 08, 2023
  • BAJETI YA KISHINDO KINONDONI

    February 02, 2023
  • KINONDONI IMETOA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 2.5 KWA VIKUNDI 115 VYA WAJASIRIAMALI BILA RIBA

    January 31, 2023
  • WITO UMETOLEWA KWA WAFANYABIASHARA KUREJEA MAENEO RASMI WALIYOTENGEWA

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MCHUMI AWEKA WAZI MCHANGANUO WA BAJETI YA MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.