• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Matukio ya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo cha mijini
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji, mifugo na uvuvi
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Baraza la Madiwani
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

KINONDONI YAENDESHA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA

Tarehe iliyowekwa: February 23rd, 2022

Manispaa ya Kinondoni imeandaa mafunzo ya siku moja kwa Watendaji wa Kata na Mitaa yenye lengo la kuwawezesha kutekeleza jukumu la msingi la utambuzi wa maeneo pamoja na barabara ili zoezi la anwani za makazi liweze kukamilika kwa wakati na ufanisi.

Akifungua semina hiyo ya siku moja kwa Watendaji hao Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw. Salum Yusuph amesema Watendaji wa Kata na Mitaa ndio watu muhimu katika kufanikisha azma nzima hasa ikizingatiwa utekelezaji wa majukumu yao unagusa wananchi moja kwa moja.

"Ninyi Watendaji mnaotekeleza majukumu yenu kwenye Kata na Mitaa, huko ndio mnaojua eneo hili ni lipi na barabara hii ni ya wapi, ndio mnaotekeleza majukumu yanayogusa wananchi moja kwa moja, hivyo kwa zoezi hili bila nguvu yenu, uwajibikaji wenu, ufanisi wake utakuwa mgumu. Niwaombe mshiriki uwezeshaji huu wa siku moja kwa ufanisi ili tuweze kwenda sawa kufikia lengo kusudiwa".  Amesema Salum Yusuph.

Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo pia amezitaja faida zitakazopatikana baada ya kukamilika kwa zoezi zima la anwani za makazi kuwa ni kurahisisha zoezi la sensa linalotarajiwa kuanza mwezi wa nane, litarahisisha upatikanaji wa huduma, litasaidia katika ukuaji wa uchumi, ulinzi na usalama wa mtu binafsi na Taifa, litatoa mwelekeo wa upatikanaji wa fursa mbalimbali na kusaidia utambuzi wa nyumba na idadi ya wakazi wa eneo husika.

Alpokuwa akitambulisha mada zilizoandaliwa kwa Watendaji hao wa Kata na Mitaa, Mwenyekti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Afisa Ardhi Mteule Ndg. Geofrey Mwamsojo amesema mafunzo haya yatarahisisha utekelezaji wa zoezi hili na kuwataka watendaji hao kuzingatia ili waweze kukabiliana na kikwazo chochote katika ukamilishaji wake.

Mada zilizofundishwa ni pamoja na mwongozo wa mfumo wa anwani za makazi,  ukusanyaji wa taarifa, manufaa ya mfumo wa anwani, majukumu ya kila mmoja, pamoja na utoaji na upatikanaji wa taarifa.

Mafunzo haya ya siku moja yamehusisha Watendaji wa Kata zote 20 na Mitaa 106.


Imeandaliwa na

Kitengo Cha Habari na Uhusiano.

Manispaa ya Kinondoni.


Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI KWA VITENDO (PRACTICAL) June 30, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KWA NAFASI YA DEREVA DARAJA II June 29, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO ULIOFANYIKA TAREHE 28 JUNI, 2022 June 28, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 20, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • UHUSIANO WA DSM NA HAMBURG WAFANIKISHA UZINDUZI KIWANDA CHA MBOJI

    June 30, 2022
  • VIKUNDI 286 VYA WANUFAIKA WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 VYAPATIWA MAFUNZO

    June 20, 2022
  • MAFUNZO KAZI YA MFUMO WA UTOAJI, USIMAMIZI WA MIKOPO YA ASILIMIA 10

    June 18, 2022
  • KINONDONI YAPONGEZWA KWA UJENZI WA KIWANJA CHA MICHEZO

    May 26, 2022
  • Tazama zote

Picha Jongefu

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.