• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Matukio ya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo cha mijini
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji, mifugo na uvuvi
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Baraza la Madiwani
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Umma
  • Mifumo
    • NaPA
    • eMrejesho

KINONDONI KUFIKIA TAKRIBANI WANANCHI MILIONI 1.2, UGAWAJI WA DAWA KINGA NA TIBA YA MABUSHA NA MATENDE

Tarehe iliyowekwa: December 13th, 2018

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo, alipokuwa mwenyekiti katika kikao cha kamati ya Afya ya msingi kilichofanyika leo kwa lengo la kupitia na kujadili maswala ya msingi ya utekelezaji wa huduma za afya, ikiwemo utekelezaji wa kampeni ya ugawaji dawa kingatiba kwa magonjwa ya mabusha na matede.

Amesema  katika kampeni hii inayotarajia kuanza tarehe 15/12/2018 hadi tarehe 20/12/2018, Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto,  kupitia kitengo cha magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, imelenga kufikia wananchi takribani milioni 1.2, katika kata zake 20, na mitaa 106.

"Kwanza niseme tunaishukuru Serikali kupitia kitengo husika cha kampeni hii, kwani ,Taifa lenye tija, ni taifa la watu wenye afya bora, hivyo hatuna budi sisi kama kamati kuhakikisha wananchi wanahamasika na wanajitokeza kwa wingi kupata kingatiba hii, na hii itatokana na elimu madhubuti itakayotolewa nanyi, kwa njia zilizosahihi na kuwafikia wananchi kwa usahihi na wakati"Amesisitiza Chongolo

Akieleza hatua zilizochukuliwa hadi sasa kuhusiana na kampeni hiyo, Mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika Manispaa hiyo,  Dr.Neema Mlole amesema wagawa dawa takribani 392, wanaotakiwa kugawa dawa za kinga wameshapatiwa mafunzo, zoezi la ugawaji dawa za kingatiba za kuzuia magonjwa ya kichocho na minyoo kwa ngazi ya Wilaya zimeshafanyika, usambazaji wa dawa na vifaa maalumu umeshafanyika, pamoja na kufanyika kwa maandalizi mazuri ya usimamizi wa zoezi zima.

Katika hatua nyingine mratibu wa zoezi la lishe Manispaa ya Kinondoni Bi Emiliana Sumaye, alipotakiwa kuzungumzia  zoezi hilo  amesema lengo ni kutoa huduma jumuishi za kinga bila malipo kwa ajili ya kuimarisha afya ya mtoto na kuyataja  mafanikio yake kuwa ni kupata ushirikiano mkubwa kwa timu ya wataalamu juu ya utekelezaji wake na pia kufikia asilimia 102% ya utoaji wa matone ya vitamin A katika vituo vya afya na zahanati.

Aidha Bi Sumaye pia ameainisha changamoto zilizojitokeza katika uendeshaji wa zoezi hilo kuwa  ni ufinyu wa bajeti, ukosefu wa vifaa tiba, pamoja na upungufu wa watoa huduma  juu ya matibabu ya utapiamlo mkali.

Kamati hiyo iliyohudhuriwa na mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na wakuu wa idara na vitengo, pia imejadili  taarifa za utekelezaji wa zoezi la utoaji wa kingatiba za magonjwa ya matende na mabusha na  taarifa ya utekelezaji wa zoezi la mwezi lishe la utoaji wa Vitamin A.

Imeandaliwa na

Kitengo cha Uhusiano na habari.

Manispaa ya kinondoni.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 13, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA DEREVA DARAJA II September 21, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI (TAREHE 20 SEPTEMBA, 2021) September 21, 2021
  • TANGAZO LA KUWAPANGA WAFANYABISHARA KATIKA MAENEO RASMI September 28, 2021
  • Tazama zote

Habari mpya

  • BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU KINONDONI LAFANYIKA LEO

    May 18, 2022
  • KINONDONI KUFIKIA WATOTO TAKRIBANI 156871 KAMPENI YA SIKU NNE CHANJO YA POLIO KITAIFA

    May 18, 2022
  • MWENGE WA UHURU KINONDONI 2022, WAPITIA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI TAKRIBANI BILIONI 3.9 FEDHA ZA KITANZANIA

    May 10, 2022
  • MEYA KINONDONI AFUTURISHA

    April 27, 2022
  • Tazama zote

Picha Jongefu

POSHO MADIWANI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.