• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Matukio ya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo cha mijini
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji, mifugo na uvuvi
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Baraza la Madiwani
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Umma
  • Mifumo
    • NaPA
    • eMrejesho

DC HAPI AMALIZA MGOGORO SUGU WA ARDHI NAKASANGWE.

Tarehe iliyowekwa: August 2nd, 2017


 NI MGOGORO UNAOHUSU WANANCHI ZAIDI YA  3200

 MGOGORO HUUUMEDUMU KWA TAKRIBANI MIAKA 13.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi leo amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa maeneo ya Nakasangwe, Nakalekwa na kuwapa ujumbe kuwa mgogoro wa ardhi uliodumu eneo hilo kwa takriban miaka 13  sasa suluhu yake imepatikana. 

 Hapi ameyasema hayo  ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa utatuzi wa migogoro ya ardhi Wilayani Kinondoni  ambapo ofisi yake ilizikutanisha pande mbili za wenye mashamba na wakazi ambazo kwa miaka kadhaa zimekua kwenye mgogoro mkubwa na kufanya nao mazungumzo yaliyoweka msingi mzuri wa kumaliza mgogoro huo.

 Aidha Mh. Hapi amewahakikishia wananchi hao kutokuwa na wasiwasi na kwamba serikali Wilayani Kinondoni imeamua kutumia falsafa ya
 "Pata kidogo poteza kidogo" (win win solution), ili kumaliza mgogoro huo baina ya pande mbili na kurejesha hali ya amani katika eneo hilo.

 "Tumeamua sasa eneo hili lote lipimwe viwanja, ili wakazi wote mliohakikiwa kila mmoja apate kipande cha ardhi cha kuishi na familia yake na viwanja vinavyobaki wapate wenye mashamba. Hii ndiyo njia pekee ya kuweza kuwafanya muishi kwa amani katika mji uliopimwa na kupangwa vizuri."
 Alisema DC Hapi

 Hali kadhalika, Hapi aliwaeleza wananchi hao kuwa katika eneo hilo zaidi ya viwanja 6000 vitapatikana na hivyo kuwatoa shaka kuwa wakazi wote zaidi ya 3000 waliohakikiwa kila mmoja atapata ardhi iliyopimwa huku wenye mashamba nao wakipata viwanja vitakavyobakia ili waweze kuviendeleza au kuviuza vikiwa na hati miliki.

 DC Hapi ameongeza kuwa  kazi ya upimaji wa ardhi katika eneo hilo inatarajiwa kuanza haraka na kumalizika ndani ya kipindi cha miezi mitatu chini ya kampuni ya Afro Map ambayo pande mbili zimeichagua kufanya kazi hiyo.

 "Nawapa kampuni hii miezi mitatu tu, kazi ya upimaji iwe imekamilika eneo hili ili wananchi wangu waishi kwa amani wakijua serikali yao ipo kuwasaidia."
 Alisema DC.

 Mgogoro wa Nakasangwe ulianza mwaka 2004 na hivyo kudumu kwa miaka takribani 13 kipindi ambacho kilitawaliwa na chuki, uhasama na uadui mkubwa baina ya wenye mashamba na wananchi waliovamia mashamba hayo na kusababisha  watu kadhaa kupoteza maisha katika mgogoro huo.

 Wananch wote wanaounda pande mbili za mgogoro wamemshukuru DC Hapi na kushikana mikono kama ishara ya mwisho wa mgogoro huo na mwanzo mpya.

 Imetolewa na
 Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
 Wilaya ya Kinondoni.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 13, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA DEREVA DARAJA II September 21, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI (TAREHE 20 SEPTEMBA, 2021) September 21, 2021
  • TANGAZO LA KUWAPANGA WAFANYABISHARA KATIKA MAENEO RASMI September 28, 2021
  • Tazama zote

Habari mpya

  • BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU KINONDONI LAFANYIKA LEO

    May 18, 2022
  • KINONDONI KUFIKIA WATOTO TAKRIBANI 156871 KAMPENI YA SIKU NNE CHANJO YA POLIO KITAIFA

    May 18, 2022
  • MWENGE WA UHURU KINONDONI 2022, WAPITIA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI TAKRIBANI BILIONI 3.9 FEDHA ZA KITANZANIA

    May 10, 2022
  • MEYA KINONDONI AFUTURISHA

    April 27, 2022
  • Tazama zote

Picha Jongefu

POSHO MADIWANI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.