• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fukwe na Visiwa
    • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Matukio ya Utalii
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Iliyopangwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio

Mzimuni

HISTORIA FUPI:

Kata ya Mzimuni ndio Kata kongwe ambayo ndiyo iliyobeba watu mashuhuri, waasisi wa Chama Tawala, na wapigania Uhuru waliopanga mikakati ya kuikomboa Tanganyika na kuwa huru. Mwalimu Nyerere alijenga nyumba na kuishi hapo ambapo kwa sasa ni Makumbusho ya Taifa.

Viongozi wengine wa kitaifa waliokuwa wakiishi hapo ni pamoja na: - Rashid Mfaume Kawawa, Abdul Kandoro, Ndugu Kambona, Sheikh Amri Abeid Kaluta, Mzee Songambele, Lucy Lameck, Chifu Abdallah Fundikira, Tewa said Tewa.      

ASILI YA JINA LA MZIMUNI: - Jina la Mzimuni limetokana na uwepo na msitu na pori kubwa lenye wanyama wakali pamoja na nyoka wengi, na ndani ya eneo hilo kulikuwa na visima viwili vya chemchem. Kimoja kati ya visima hivyo kilikuwa kinatoa maji mengi ambayo watu walikuwa wakiyatuia kwa kunywa, kuoga (kuondosha mikosi/matatizo mbalimbali) mfano wenye ugonjwa na kwa matambiko ya kijadi.

Kisima hiko kilikuwa na maajabu wakati mwingine maji yake hua mekundu au meusi, na ikalazimika watu wasiende katika kisima hiko kati ya saa 6 hadi 8 mchana, na saa 12 jioni na kisima kingine maji yake yalikua yakitoka katikati ya mwembe mkubwa, na kilikuwa na nyoka mkubwa, ambapo watu na wanyama wakifika katika kisima hiko, walikua wakipotea.

Mmoja wa wazee marufu Bwana Ramadhani Madogoli, ndiye alikua akitumia sana eneo hilo kwa shughuli za matambiko, ikiwemo ngoma ya asili iitwayo Mganda. Pia kulikua na mwembe ng'ongo mkubwa na katikati ya shina la mwembe huo palikua na tundu la wazi ambapo wakati mwingine unaweza kukuta chakula au fedha. 

Lakini pia palikuwa na makaburi ya asili ambayo nyakati za usiku kulikuwa na mambo ya ajabu.  Na wakazi wa eneo hilo walikua wakisoma shule ya Mzizima, ndipo baadaye Wazungu wakataka kujenga hospitali, lakini wazee walikataa na kuomba wajengewe shule, na hatimaye eneo hilo likajengwa shule ya msingi na kuitwa Mzimuni ambayo ilikwepo kabla ya uhuru miaka ya 1954. Hospitali/Kituo cha Afya kikajengwa eneo la Magomeni na miongoni mwa watu maarufu waliosoma shule ya msingi Mzimuni ni: -  Ramadhani Dau, Juma Kapuya, Saidi Mwambungu n.k

Madiwani wa kwanza waliongoza Kata hii ni pamoja na Mzee Luyaya, Mzee Chambuso, Ally Bwamkuu (2000) na Abdulkarim Mtoni (2000 – 2010).

 

IDADI YA MITAA:

Kata ya Mzimuni ina jumla ya mitaa minne (04) ya Kiserikali ambayo ni: -

  1. Idrisa
  2. Makumbusho
  3. Mwinyimkuu
  4. Mtambani


HALI YA ELIMU KATIKA KATA:

Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya awali, msingi na sekondari za serikali na binafsi.


SHULE ZA MSINGI ZA SERIKALI:

Kata ya Mzimuni inazo shule za msingi mbili (02) za serikali kama ifuatavyo: -

  1. Shule ya msingi Mzimuni
  2. Shule ya msingi Mikumi

 

SHULE ZA AWALI ZA NA MSINGI ZA BINAFSI:

Kata ya Mzimuni inazo shule za awali na msingi mbili (02) za binafsi kama ifuatavyo:-

  1. Shule ya msingi Shekhat Hissa
  2. Shule ya msingi Izza Juniour


SHULE YA SEKONDARI YA SERIKALI:

Kata ya Mzimuni ina shule moja (01) ya sekondari ya serikali ijulikanayo kwa jina la Mzimuni sekondari.  


SHULE YA SEKONDARI YA BINAFSI:

Kata ya Mzimuni ina shule moja (01) ya sekondari ya serikali ijulikanayo kwa jina la Nur Islamic Seminari  


HALI YA AFYA:

Hali ya Afya katika Kata ya Mzimuni ni ya kuridhisha kwani ina Hospitali ya binafsi na Zahanati za serikali na binafsi.


HOSPITALI ILICHOPO KATA YA MZIMUNI:

Kata ya Mzimuni ina Hospitali moja (01) ya binafsi inayojulikana kwa jina la Hospitali ya Mikumi.


ZAHANATI ZILIZOPO KATA YA MZIMUNI:

Zahanati zilizopo katika Kata ya Mzimuni ni nne (04) ambapo 1 kati ya idadi tajwa ni ya serikali inayojulikana kwa jina la Zahanati ya Mzimuni na za binafsi ni: Mosha dental clinic, Herbal clinic ya Wachina, na Omega dental clinic.


HALI YA MIUNDOMBINU YA BARABARA:

Hali ya miundombinu ya barabara katika Kata ya Mzimuni inaridhisha. Kata nzima ina barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita 3.


MAHUSIANO NA WADAU WA MAENDELEO:

Mahusiano na wadau wa maendeleo yapo vizuri, ambapo Kata inapata ushirikiano toka kwa wadau wafuatayo: - Benki ya NMB, TOTAL Petrol Station, HOTEL TRAVETINE, NORTHELAND HOTEL, BUTIAMA HOTEL, MIKUMI IN HOTEL, KISUMA BAR AND LODGE n.k

Matangazo

  • TANGAZO KUHUSU WAFUGAJI WENYE MIFUGO INAYOZURURA OVYO January 30, 2023
  • TANGAZO ULIPAJI WA TOZO January 26, 2023
  • TANGAZO KWA WAOMBAJI WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA MAPATO YA NDANI November 24, 2022
  • MABADILIKO YA SIKU YA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WA MAUDHUI, WASIMAMIZI WA TEHAMA NA MAKARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 July 28, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • PUNGUZENI MATUMIZI YA KARATASI-NDUMBARO

    February 08, 2023
  • BAJETI YA KISHINDO KINONDONI

    February 02, 2023
  • KINONDONI IMETOA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 2.5 KWA VIKUNDI 115 VYA WAJASIRIAMALI BILA RIBA

    January 31, 2023
  • WITO UMETOLEWA KWA WAFANYABIASHARA KUREJEA MAENEO RASMI WALIYOTENGEWA

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MCHUMI AWEKA WAZI MCHANGANUO WA BAJETI YA MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.