• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fukwe na Visiwa
    • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Matukio ya Utalii
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Iliyopangwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio

Msasani

KATA YA MSASANI:

Kata ya Msasani ilikuwa inajulikana kwa jina la Mikoroshoni ambalo lilitokana na uwepo wa mikorosho mingi kwa wakati huo. Asili ya jina la Kata ya Msasani inasadikiwa kuwa ni kutokana na mtu maarufu aliyeishi maeneo hayo kipindi hicho aitwaye Mussa Hassan, na kutokana na wenyeji wa eneo hilo ambao walikuwa ni kabila la Wamakonde kushindwa kutamka kwa usahihi jina Mussa Hassan na kutamka Mucha Hachani na mwisho watu wakaanza kutamka Msasani.


IDADI YA MITAA ILIYOPO KWENYE KATA:

Kata ya Msasani ina mitaa mitano (05) kama ifuatavyo:-

1.    Mtaa wa Oysterbay

2.    Mtaa wa Masaki

3.    Mtaa wa Bonde la Mpunga

4.    Mtaa wa Makangira

5.    Mtaa wa Mikoroshoni

         

HALI YA ELIMU KATIKA KATA:

Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya awali, msingi na sekondari za serikali na binafsi.


SHULE ZA AWALI NA MSINGI ZA SERIKALI:

Kata ya Msasani inazo shule za msingi za serikali tano (05) ambazo ni

  1. Shule ya msingi Msasani A
  2. Shule ya msingi Msasani B
  3. Shule ya msingi Mbuyuni
  4. Shule ya msingi Bongoyo
  5. Shule ya msingi Oysterbay

Shule zote hizi zina miundombinu ya maji safi na umeme. Shule ya msingi Oysterbay imepandishwa daraja na kuwa shule ya mchepuo wa kiingereza "English Medium". Aidha kuna vitengo vya kuhudumia watoto wenye mahitaji maalumu (Disabilities), katika shule ya msingi Msasani A na Mbuyuni.


SHULE  YA AWALI YA BINAFSI:

Kata ya Msasani pia ina shule moja ya awali ya binafsi ijulikanayo kwa jina: Lady Chesham.


SHULE  ZA MSINGI ZA BINAFSI:

Kata ya Msasani inazo pia shule tisa za msingi za binafsi ambazo ni:-

  1. Shule ya msingi ya Drive Inn Msasani Islamic
  2. Shule ya msingi ya Penisula Good Sanitarian
  3. Shule ya msingi Peninsula
  4. Shule ya msingi Al Irshad
  5. Shule ya msingi Drive Inn
  6. Shule ya msingi Dar Independence
  7. Shule ya msingi Genesis
  8. Shule ya msingi French
  9. Shule ya msingi Leaders Rabbit


SHULE YA SEKONDARI YA SERIKALI:

Kata ya Msasani inayo shule moja ya sekondari ambayo ni ya serikali iitwayo Oysterbay.


SHULE ZA SEKONDARI ZA BINAFSI:

Kata ya Msasani inazo pia shule za sekondari za binafsi tano kama zifuatazo;-

  1. Sekondari ya Tanganyika International
  2. Sekondari ya Dar es Salaam
  3. Sekondari ya Good Sanitarian
  4. Sekondari ya Islamic
  5. Sekondari ya Siera


VYUO VYA ELIMU YA KATI:

Kata ya Msasani ina Chuo cha Elimu  ya Kati cha Serikali kimoja (1) ambacho ni Chuo cha Tanesco Masaki. Vilevile kuna chuo kimoja cha binafsi ambacho ni Don Bosco VTC.


HALI YA AFYA:

Hali ya afya katika Kata ya Msasani ni ya kuridhisha kwani inayo hazina ya kutosha ya Hospitali, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati za serikali na binafsi.


HOSPITALI ZA BINAFSI ZILIZOPO KATA YA MSASANI:

  1. Hospitali ya Msasani Penisula
  2. Hospitali ya London
  3. Hospitali ya Santas
  4. Hospitali ya Oysterbay
  5. Hospitali Sali International


VITUO BINAFSI VYA AFYA VILIVYOPO KATA YA MSASANI:

  1. Kituo cha afya cha ABC Dental Centre.
  2. Kituo cha afya cha Aga Khan Medical Centre.
  3. Kituo cha afya cha St. LAURENT Diabetic Centre.


ZAHANATI ZA SERIKALI ZILIZOPO KATA YA MSASANI:

  1. Zahanati ya Mikoroshini
  2. Zahanati ya Polisi Oysterbay


ZAHANATI ZA BINAFSI ZILIZOPO KATA YA MSASANI:

  1. Kidney Care
  2. TPM Dispensary
  3. Bonde la Mpunga Dispensary
  4. New Msasani Dispensary
  5. Oysterbay Dispensary.
  6. Sanitarian Dispensary
  7. St. Benedict Dispensary
  8. New Vision Eye Clinic
  9. Divine Grace Dental Clinic
  10. Letus Physiotherapy Clinic
  11. Dental Studio Clinic
  12. Premier Care Clinic
  13. Elite Dental Clinic


HALI YA MIUNDOMBINU YA BARABARA:

Hali ya miundombinu ya barabara Kata ya Msasani ni ya kuridhisha kutokana na kuwa na mtandao mkubwa wa barabara za kiwango cha lami na chache ni za kiwango cha changarawe ambazo asilimia kubwa zipo katika hali nzuri zinazopitika katika misimu yote ya mwaka.


USAFI WA MAZINGIRA:

Usafi wa mazingira wa Kata hii ni wa kuridhisha kwani kila Mtaa una Wakandarasi wa usafi wanaozoa taka kwa wakati na hutumia mashine za kielektroniki.


MAHUSIANO NA WADAU:

Mahusiano ya wadau wa maendeleo na uongozi wa Kata na Mitaa ni mzuri, kwani wako mstari wa mbele kuchangia shughuli za kijamii na miradi ya maendeleo.


MRADI WA KUJIVUNIA:

Mradi wa kujivunia katika Kata ya Msasani ni ujenzi wa mfereji mkubwa wa maji ya mvua kutoka Mayfair hadi baharini ambao unasaidia kuondoa kero ya mafuriko katika Kata ya Msasani.


MIPANGOMIJI:

Kata ya Msasani eneo lake kubwa limepimwa na sehemu ndogo ya makazi holela ambako hakujapimwa hivyo kupelekea watu kupima wenyewe kunakoleteleza changamoto ya miundombinu ya barabara za mitaa.


Matangazo

  • TANGAZO KUHUSU WAFUGAJI WENYE MIFUGO INAYOZURURA OVYO January 30, 2023
  • TANGAZO ULIPAJI WA TOZO January 26, 2023
  • TANGAZO KWA WAOMBAJI WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA MAPATO YA NDANI November 24, 2022
  • MABADILIKO YA SIKU YA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WA MAUDHUI, WASIMAMIZI WA TEHAMA NA MAKARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 July 28, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • PUNGUZENI MATUMIZI YA KARATASI-NDUMBARO

    February 08, 2023
  • BAJETI YA KISHINDO KINONDONI

    February 02, 2023
  • KINONDONI IMETOA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 2.5 KWA VIKUNDI 115 VYA WAJASIRIAMALI BILA RIBA

    January 31, 2023
  • WITO UMETOLEWA KWA WAFANYABIASHARA KUREJEA MAENEO RASMI WALIYOTENGEWA

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MCHUMI AWEKA WAZI MCHANGANUO WA BAJETI YA MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.