Kitengo cha sheria kina majukumu mengi katika Halmashauri. miongoni mwa hayo ni kama yafuatayo;
Kumshauri Mkurugenzi juu ya masuala yote yahusuyo sheria katika Halmashauri.
Kushauri Idara nyingine zote zilizopo katika Halmashauri juu ya masuala yote yanayohusu sheria
Kutunga na kuandaa sheria ndogo ndogo za Halmashauri kwa ajili ya kuwezesha uendeshaji wa shughuli za kila siku za Halmashauri
Kusimamia na kuiwakilisha Halmashauri katika mashauri yote ambayo Halmashauri inahusika
Kupitia mikataba yote inayohusu Halmashauri
Kuunda na kusimamia mabaraza yote ya Kata yaliyopo ndani ya Halmashauri
Kutoa msaada wa kisheria kwa jamii yote iliyopo ndani ya Halmashauri
Kusimamia suala zima la ulinzi wa mali za Halmashauri
Kusimamia na kufuatilia wadaiwa wote wa Halmashauri
Kumshauri Mkurugenzi juu ya mbinu bora za ukusanyaji wa mapato na uanzishwaji wa vyanzo vipya vya mapato kwa ustawi wa Halmashauti
Kusimamia utekelezaji wa sheria za Nchi.
Kupitia kutumia na kusimamia mikataba ya Halmahauri.
Kuratibu shughuli za Ulinzi na usalama wa Manispaa
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255 22 2170173
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.