• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fukwe na Visiwa
    • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Matukio ya Utalii
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Iliyopangwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio

KUFAHAMU TARATIBU ZA UTOAJI WA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA MANISPAA YA KINONDONI

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatekeleza programu ya mfuko wa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kama ilivyo kwa Halmashauri zote nchini kufuatia agizo la Serikali la mwaka 1998 kuwa Halmashauri zote nchini zianzishe mfuko huo kwa kutenga asilimia 10% ya mapato yake ya ndani.

Halmashauri imekuwa ikifuata mwongozo wa mikopo kwa kuhakikisha inaboresha mfumo huo bila kukiukwa ili kuimarisha umiliki wa fedha za mfuko wa Halmashauri.


LENGO LA KUBORESHA MFUMO

•    Kuimarisha umiliki wa fursa ya mikopo ya Manispaa.

•    Kuondoa mgongano wa mikopo kati ya Manispaa na wakala.

•    Kuimarisha utambulisho wa walengwa kwa kuzingatia mwongozo.

•    Kuondoa gharama/udhamini wa wakala (10%) ya fedha za mikopo.


Kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 utaratibu wa utoaji wa mikopo utakuwa kama ifuatavyo:-

Mchakato wote wa utoaji wa mikopo utasimamiwa na kuratibiwa na Halmashauri kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, kuanzia uhamasishaji wa mikopo, kuainisha vikundi hadi hatua ya vikundi kupata mikopo yao na kufanya marejesho


MCHAKATO WA UKOPESHAJI

•    Uhamasishaji

•    Uainishaji wa vikundi

•    Majukumu ya wadau/viongozi

•    Kujenga uwezo wa vikundi

•    Ukopeshaji

•    Urejeshaji

•    Usimamizi na ufuatiliaji.


UHAMASISHAJI

•    Viongozi wa ngazi mbalimbali za uongozi watafanya uhamasishaji juu ya mikopo ya masharti nafuu kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

•    Baada ya Uhamasishaji, wananchi wataelekezwa kwenda kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata husika ili kuendelea na hatua zinazofuata.

•    Pia utafanyika uhamasishaji wa uundaji wa vikundi na kuvijengea uwezo ili kuwa na sifa.

Baada ya uhamasishaji na uundwaji wa vikundi, zoezi litakalofuata ni kuvitambua vikundi ambavyo vitakuwa na sifa ya kukopesheka kwa kufanya yafuatayo:-

•    Vikundi vya wakopaji watajiorodhesha katika ofisi zao za Kata kwa Afisa Maendeleo ya Jamii.

•    Kuainisha na kuchambua vikundi vinavyostahili kupewa mikopo.

•    Kutoa hati ya usajili kwa vikundi.


UNITI YA USIMAMIZI

Katika ngazi ya Manispaa, kutakuwa na Uniti ya Mikopo ambayo itakuwa na:-

1.    Afisa Maendeleo ya Jamii - Mratibu

2.    Mhasibu

3.    Mwanansheria

4.    Mchumi.


MAJUKUMU YA WADAU /VIONGOZI WA KATA

•    Viongozi katika ngazi na kada mbalimbali watafanya uhamasishaji kwa ajili ya wananchi kutambua fursa ya mikopo.

•    Ofisi ya Mtaa itahusika na kuwatambulisha wakopaji na kuthibitisha ukaazi wao katika mitaa yao.

•    Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watahusika na kupitisha majina na vikundi vinavyostahili kupatiwa mikopo.

•    Afisa Maendeleo ya Jamii atahusika na uratibu wa zoezi la kuainisha vikundi vinavyostahili kupata mikopo, kujenga uwezo wa vikundi na kuviwasilisha ofisini uratibu wa mikopo.


MAMBO YA KUZINGATIA

•    Umri wa mkopaji - kuanzia miaka 18.

•    Wanaume iwe ni kati ya miaka 18 hadi 35

•    Shughuli ambazo zitapewa kipaumbele ni pamoja na viwanda vidogo vidogo na vikundi vyenye wanachama wenye ulemavu/vikundi vya wenye ulemavu.

•    Wakopaji kuwa na utambulisho wa makazi kwa kuwasilisha barua ya Mtendaji wa Mtaa anakotokea.

•    Vikundi kuwa na Katiba.

•    Kusaini mkataba ulioambatishwa majina ya wana kikundi ukionesha malengo ya mkopo ya kila mwana kikundi kwa kila awamu ya mkopo anaoomba.


KUJENGA UWEZO WA VIKUNDI

•    Kila kikundi kitalazimika kufungua Akaunti katika Benki itakayokubaliwa.

•    Vikundi vitakavyokuwa na sifa ya kukopeshwa vitapatiwa mafunzo juu ya uwekaji wa akiba, kuandaa katiba, ukopaji na urejeshaji wa mikopo.

•    Afisa Maendeleo ya Jamii atawasilisha taarifa ya vikundi kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata kwa ajili ya uchambuzi wa hatua ya awali.


UKOPESHAJI

•    Kila mwanakikundi ataainisha kiasi cha mkopo anachohitaji na muda wa marejesho.

•    Mikopo ya wanakikundi itajumlishwa na kupata kiasi cha mkopo wa kikundi.

•    Kutokana na mahitaji ya kila mwanakikundi, itapigwa hesabu ya rejesho kwa wiki.

•    Kila kikundi kitaingiziwa fedha katika akaunti katika Benki itakayokubaliwa.


UREJESHAJI WA MIKOPO

•    Kila mwanakikundi atarejesha kiasi cha rejesho lake kwa mkusanyaji wa fedha wa kikundi.

•    Fedha zikishakusanywa, mkusanya fedha atapeleka marejesho kwenye akaunti maalum ya Manispaa.

•    Mkusanya fedha atawasilisha passbook pamoja na payslip kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata husika.


NB: Kila kikundi kitalazimika kusaini mkataba wa kumdhamini mwanakikundi mwenzao na kuhakikisha wanabeba deni la mwanakikundi mwenzao pindi anaposhindwa kulipa deni lake.


USIMAMIZI NA UFUATILIAJI

•    Mfumo wa marejesho utatumika kwa kushirikiana na Maafisa wa Benki kupitia vituo vitakavyoainishwa na Kata.

•    Kata itakayofanya vizuri kwa wakopaji wake kurejesha mikopo kwa zaidi ya asilimia tisini na tano (95%) itaongezewa kiwango cha fedha za mikopo.

•    Kata ambazo hazitafanya vizuri hazitaongezewa fedha nyingine kwa mwaka unaofuata hadi marejesho ya fedha za awali yafikie zaidi ya asilimia tisini na tano (95%).

•    Kila mwisho wa mwaka wa fedha itafanyika tathmini ya kuzitambua Kata ambazo zimefanya vizuri na zile ambazo hazikufanya vizuri.

•    Taarifa ya mikopo itatolewa katika taarifa ya utekelezaji wa miradi kila robo ya mwaka katika Baraza la Madiwani.


MASWALA YA KUZINGATIA

•    Kushirikiana na Benki itakayopendekezwa kwa ajili ya kurahisisha ufuatiliaji wa marejesho.

•    Benki zinazopendekezwa ni TWB, NMB, CRDB, TPB, na DCB kwani Benki hizi ni za Serikali na pia zina huduma kwa ajili ya vikundi.


UPATIKANAJI WA FEDHA

•    Inapendekezwa kuwa mikopo itolewe mara 4 kwa mwaka (mara moja kwa kila robo ya mwaka).

•    Fedha zilizokusanywa na kuchangiwa kwenye mfuko zitatolewa kwa kuzingatia uwiano kwa Kata.

Matangazo

  • KUFUTA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI March 14, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA March 13, 2023
  • TANGAZO KWA WASIOLIPIA VIWANJA BOKO DOVYA (KWA SOMJI) NA SALASALA February 15, 2023
  • MABADILIKO YA SIKU YA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WA MAUDHUI, WASIMAMIZI WA TEHAMA NA MAKARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 July 28, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • JAPAN YAIPATIA MSAADA MZIMUNI SEKONDARI

    March 15, 2023
  • VIKUNDI VYAASWA MATUMIZI SAHIHI YA MIKOPO

    February 18, 2023
  • "HAKUNA TIMU KUBWA ZAIDI YA KMC FC"

    February 18, 2023
  • ULINZI NI KIPAUMBELE KINODONI-DC SAAD

    February 12, 2023
  • Tazama zote

Picha Jongefu

VIKUNDI VILIVYOSEPA NA BILIONI 11 VYAKALIWA KOONI MANISPAA YA KINONDONI. REJESHENI...
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • TAARIFA KWA UMMA
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.