• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Matukio ya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo cha mijini
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji, mifugo na uvuvi
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Baraza la Madiwani
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

MBIO MAALUM ZA MWENGE WA UHURU, 2021

Sunday 3rd, July 2022
@Dar es Salaam

Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru 2021 kukimbizwa kwa siku 150 katika wilaya 150 za kiutawala za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania badala ya Halmashauri 195.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokutana na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kwa lengo la kutoa taarifa kwa umma kuhusu tukio la uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2021.

Mheshimiwa Mhagama alisema kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu wa 2021 ni Mbio maalum, umaalum wake pia unatokana na Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kukimbizwa katika Wilaya 150 za kiutawala tu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania badala ya Halmashauri za Wilaya 195 kama ilivyozoeleka.

“Chombo hiki sasa ni budi kikimbizwe tena nchini kote baada ya kutofanya kazi toka mwaka 2020 kutokana changamoto za Ugonjwa wa Corona, hivyo ili kiweze kurejesha matumaini kwa watanzania na kuwahimiza kuchapa kazi chini uongozi shupavu wa Serikali ya awamu ya sita inayoongwa na Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mhagama

Alifafanua kuwa, Falsafa ya Mwenge Mwenge wa Uhuru ndio chimbuko la Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa Mwaka 1964 na Azmio la Arusha la mwaka 1967.

Akinukuhu maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoyatoa mwaka 1958 wakati akihutubia kikao cha 35 cha Umoja wa Mataifa na kuyarudia tarehe 22 Oktoba, 1959 wakati akihutubia Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika (LEGCO) “Sisi watu wa Tanganyika, tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pamejaa chuki na heshima palipo na dharau”

“Ni mwaka wa 29 sasa toka Mbio za Mwenge wa Uhuru zilivyoanzishwa na waasisi wetu na umeendelea kuwa chombo muhimu kwa Taifa kwa kujenga undugu, umoja, mshikamano na kudumisha amani pote unapopita bila kujali itikadi zetu za kisiasa, dini wala makabila yetu.” alieleza

Aliongeza kuwa Mwenge wa uhuru na mbio zake zimekuwa na faida kwa taifa ikiwemo kuendelea kuhamasisha Wananchi kushirikiana na Serikali yao katika kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali za maendeleo katika nyanja za kilimo, ufugaji, Uvuvi endelevu, uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, umeme na huduma za jamii katika maeneo yote nchini na hasa katika maeneo yasiyofikika kiurahisi.

Pia Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikitumika kuelimisha wananchi katika maeneo yote nchini jinsi ya kupambana na maradhi yanayotishia ustawi wa watu wetu kama vile UKIMWI, Malaria na kuhamasisha wananchi kushiriki vita dhidhi ya Rushwa na matumizi ya Dawa za kulevya na sasa zitaichukua dhana ya Lishe bora kwa afya Imara ya Watanzania. Pamoja na njia nyingine tunazotumia kuwahamasisha wananchi wetu. Bado Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa ni njia sahihi ya kufikisha taarifa na elimu sahihi ya changomoto zinazowakabili watanzania wote.

Aidha, Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wote wa Zanzibar, kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Mwehe Zanzibar na kuungana na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kufanikisha shughuli muhimu kitaifa.

Kwa Upande wake, Kaimu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Leila Mohamed Mussa alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamefanikiwa kukamilisha maandalizi kwa asilimia 100.

“Watendaji wa Serikali zote mbili wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ufanisi wa uzinduzi hu una hivyo Mwenge huo kuanza kukimbizwa rasmi” alisema Mheshimiwa Leila

Alitumia pia fursa hiyo kuwaalika wakazi wa Makunduchi na maeneo mengine mbalimbali kujitokeza kwa wingi.

Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2021, unahusu matumizi sahisi ya TEHAMA, chini ya Kauli mbiu isemayo: “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu. Itumie kwa usahihi na Uwajibikaji”. Pamoja na Ujumbe huo, Mbio za Mwenge wa Uhuru zitaendelea kuwakumbusha na kuwahamasisha wananchi na Viongozi kote nchini, kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, ugonjwa Malaria, mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za Kulevya, Mapambano dhidi ya Rushwa na kuhamasisha Wananchi juu ya Lishe bora kwa afya imara.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI KWA VITENDO (PRACTICAL) June 30, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KWA NAFASI YA DEREVA DARAJA II June 29, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO ULIOFANYIKA TAREHE 28 JUNI, 2022 June 28, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 20, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • UHUSIANO WA DSM NA HAMBURG WAFANIKISHA UZINDUZI KIWANDA CHA MBOJI

    June 30, 2022
  • VIKUNDI 286 VYA WANUFAIKA WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 VYAPATIWA MAFUNZO

    June 20, 2022
  • MAFUNZO KAZI YA MFUMO WA UTOAJI, USIMAMIZI WA MIKOPO YA ASILIMIA 10

    June 18, 2022
  • KINONDONI YAPONGEZWA KWA UJENZI WA KIWANJA CHA MICHEZO

    May 26, 2022
  • Tazama zote

Picha Jongefu

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.