Sunday 3rd, July 2022
@Manispaa ya Kinondoni.
Manispaa ya Kinondoni imesaini mkataba wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kitakachojengwa eneo la Mabwepande na kitagharimu shilingi takriban Bilioni 5.56 hadi kukamilika kwake.
Mkataba huo umesainiwa leo na Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta na kushuhudiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo pamoja na wajumbe wengine katika tafrija iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Manispaa.
Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mh.Benjamini Sitta akisaini mkataba wa mtambo wa Kuchakata taka unaotarajiwa kujengwa mabwepnade.
Baadhi ya wadau watakaousika katika kujenga kiwanda hicho.
Wajumbe pamoja nawadauwakishuhudia zoezi zima la kutiliana saini mkataba huo
Matukio katika picha ya zoezi la kutiliana sainimkataba huo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255 22 2170173
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.