Friday 13th, September 2024
@Shule ya Msingi Bongoyo.
Manispaa ya Kinondoni imekabidhiwa Maktaba ya kisasa yenye thamani ya zaidi ya milioni themanini kutoka Korea ya Kusini kwa lengo la kuimarisha mfumo wa Elimu kwa shule za msingi utakaowajengea wanafunzi Utamaduni wa kusoma.
Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamini Sitta pamoja na Balozi wa Korea ya Kusini Nchini Tanzania Ndg Keum Young Song akikata utepe kama ishara ya makabidhiano rasmi ya maktaba ya kisasa iliyojengwa na wakorea hao shule ya Msingi Bongoyo.
Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamini Sitta(Kulia), akibadilishana jambo na Afisa Elimu Msingi Wa Manispaa Bw. Kiduma Mageni(Katikati0,, pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Bongoyo Bi. Alice Martine(Kushoto), wakati wa hafla ya makabidhiano ya maktaba hiyo.
Mstahiki Meya Manispaa ya KinondoniMh. Benjamini Sitta akifurahia jambo na Balozi wa Korea Nchini Tanzania Ndg Keum Young Song wakati wa halya ya makabidhiano ya maktaba shule ya msingi Bongoyo.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Bongoyo Bi. Alice Martine akisoma taarifa mbele ya hadhira siku ya makabidhiano ya maktaba kutoka kwa wakorea .
Balozi wa Korea ya Kusin NchiniTanzania Ngd Keum Young song akisoma taarifa mbele ya hadhira siku ya makabidhiano ya Maktaba hiyo kwa Manispaa ya Kinondoni.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Bongoyo wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano ya maktaba.
Matukio Katika Picha.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.