• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Matukio ya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo cha mijini
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji, mifugo na uvuvi
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Baraza la Madiwani
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

Bunju

HISTORIA FUPI:

Kata ya Bunju ni miongoni mwa Kata kongwe ndani ya Manispaa ya Kinondoni. Jengo la ofisi ya Kata hii lilizinduliwa tarehe 29/06/2001 na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa wa Mwaka huo ambaye ni Ndg. Fatma Juma Shomari.

Bunju imetokana na neno samaki anayeitwa jina la Bunju. Hapo awali wakazi wa eneo la Kata ya ya Bunju walikuwa wafugaji ambao walitekeleza shughuli zao za uvuvi katika bahari ya Hindi.

Eneo la kati la Kata ya Bunju lilikuwa na kijiji ambacho kulikuwa na vitongoji ambavyo mojawapo ni Mabwepande ambapo kwa sasa ni Bunju B. Lakini pia Mabwepande ilikuwa inasimamiwa na Kata ya Bunju na ilikuwa na Mitaa miwili ambayo ni Boko na Bunju A.

Kuna mchanganyiko wa makabila mbalimbali ndani ya Kata ya Bunju ikiwemo Wakwere, Wazaramo na Wandengereko.


IDADI YA MITAA:

Kata ya Bunju ina jumla ya mitaa sita (06) kama ifuatavyo:-

1.    Mtaa wa Basihaya

2.    Mtaa wa Boko

3.    Mtaa wa Dovya

4.    Mtaa wa Kilungule

5.    Mtaa wa Mkoani

6.    Mtaa wa Bunju A


HALI YA ELIMU:

Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha na wanafunzi wake hujitahidi kufikia lengo la ufaulu kwa asilimia zinazotakiwa. Kata hii inazo shule za awali, msingi na sekondari ambazo ni za serikali na za binafsi. Pia Kata ina vyuo vya elimu ya kati.


SHULE ZA AWALI NA ZA MSINGI ZA SERIKALI:

Kata ya Bunju inazo shule za awali na msingi saba (7) za serikali kama ifuatavyo: -

  1. Bunju A
  2. Kheri Missinga
  3. Ally Hapi
  4. Boko
  5. Boko NHC
  6. Mtambani
  7. Bunju Mkoani


SHULE ZA AWALI NA ZA MSINGI ZA BINAFSI:

Kata ya Bunju inazo shule za awali kumi na tano (15) za binafsi kama ifuatavyo: -

Moga, Faith, Gosheni, Siya Modern, New Hazina, Abel Memorial, Prestige, Mt. Sinai, Stamarial Salome, Daystar, Locee, Turkish Maarif, Jubilation, Rev. Fr. Jagques, Mareisuvat.


SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI:

Kata ya Bunju inazo shule tatu (03) za sekondari za serikali kama ifuatavyo: -  

  1. Boko
  2. Boko Mtambani
  3. Bunju A


SHULE ZA SEKONDARI ZA BINAFSI:

Kata ya Bunju inazo shule nane (08) za sekondari za binafsi kama ifuatavyo: -  

  1. Destine
  2. Fanaka
  3. Mianzini
  4. Stamaria
  5. Salome
  6. Lyceum
  7. John the Baptist
  8. Faith


VYUO VYA ELIMU YA KATI VYA BINAFSI:

Kata ya Bunju inavyo vyuo viwili (02) vya elimu ya kati vya binafsi.


HALI YA AFYA:

Hali ya Afya katika Kata ya Bunju ni ya kuridhisha kwani ina Vituo vya Afya na Zahanati za serikali na binafsi.


KITUO CHA AFYA KILICHOPO KATA YA BUNJU:

Kituo cha Afya kilichopo ni kimoja ambacho ni cha serkikali ambacho kinaitwa Kituo cha Afya Bunju.


ZAHANATI ZA SERIKALI KATA YA BUNJU:

Kata ya Bunju ina Zahanati mbili (02) za serikali kama ifuatavyo: -

  1. Zahanati ya Boko inayohudumia wakazi wa Mtaa wa Boko, Basihaya na maeneo ya jirani.
  2. Zahanati ya Bunju inayohudumia maeneo yote yanayozunguka Bunju na Vitongoji vyake.


ZAHANATI ZA BINAFSI KATA YA BUNJU:

Kata ya Bunju ina Zahanati nane (08) za binafsi kama ifuatavyo: -

Tobson, St. Joseph, Sandary, Med Check, Agakhan Cilinic, Arafa Vigen, Burumawe Specilied Clinic Honest, Nyota Njema


HALI YA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MIFEREJI:

Kata ya Bunju inazungukwa na barabara za lami nne ambazo ni Barabara ya Boko Chama kwenda Ununio na kutokea Kunduchi ambayo pia ina mifereji ya maji ya mvua, pia kuna barabara ya njia panda Mbweni kwenda Malindi Mbweni na ambayo pia ina mifereji na barabara nyingine kuanzia Kilungule kwenda Mbweni. Lakini pia Kata ya Bunju inapitiwa na barabara kubwa ya Bagamoyo kwa mitaa yote sita.


HALI YA USAFI NA MAZINGIRA:

Hali ya usafi wa Kata ya Bunju ni wa kuridhisha, kwani mitaa yote sita inayo Wakandarasi wanaozoa taka na kusafirisha kwenda dampo.


MAHUSIANO NA WADAU:

Katika Kata ya Bunju, mdau mkubwa wa maendeleo ni kiwanda cha saruji cha Wazo ambacho mara kadhaa kimekuwa kikisaidia maendeleo katika mitaa ya Basihaya na Boko hasa katika kusaidia vifusi vya barabara, vyandarua na mazingira. Wadau wengine wanaosaidia katika Kata ni pamoja na: BARRIEL SHELI,  ATN SHELI, APC, OILCOM SHELI, GUDAL SHELI, TOOTHPICK INDUSTRY LTD, DSN ENERGY (T) LTD (KIWANDA CHA MKAA), COLD BREWERIES  ARIES, PRODUCT AZURA  KIWANDA  CHA POMBE), KIWANDA CHA GYPSUM.


MIRADI YA KUJIVUNIA:

Kata ya Bunju inajivunia hasa katika miradi ya elimu kwani pamoja na kuwa na shule nne za msingi na shule mbili za Sekondari bado imeanzisha ujenzi mpya wa shule ya msingi katika mtaa wa Mkoani.


HALI YA MAENDELEO YA WATU NA MAKAZI:

Hali ya maendeleo ya watu na makazi inakua kwa kasi kwa kuwa watu wengi wamejenga nyumba za kisasa hasa katika eneo la mradi wa viwanja 2000 (Bunju Beach), na eneo la Boko beach ambako kuna miundombinu yote ya mipangomiji.

Pia katika maeneo yasiyopimwa ujenzi unafanyika kwa kasi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI May 24, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA DEREVA DARAJA II September 21, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI (TAREHE 20 SEPTEMBA, 2021) September 21, 2021
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIKUNDI 286 VYA WANUFAIKA WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 VYAPATIWA MAFUNZO

    June 20, 2022
  • MAFUNZO KAZI YA MFUMO WA UTOAJI, USIMAMIZI WA MIKOPO YA ASILIMIA 10

    June 18, 2022
  • KINONDONI YAPONGEZWA KWA UJENZI WA KIWANJA CHA MICHEZO

    May 26, 2022
  • BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU KINONDONI LAFANYIKA LEO

    May 18, 2022
  • Tazama zote

Picha Jongefu

POSHO MADIWANI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.