KATA YA WAZO.
Asili ya jina la Kata ya Wazo ni kutokana na umaarufu wa Kiwanda cha Wazo.
IDADI YA MITAA.
Kata ya Wazo inajumla ya Mitaa nane kama ifuatavyo:-
1. Mtaa wa Salasala
2. Mtaa wa Kilimahewa
3. Mtaa wa Kilimahewa Juu
4. Mtaa wa Wazo
5. Mtaa wa Kisanga
6. Mtaa wa Mivumoni
7. Mtaa wa Madale
8. Mtaa wa Nyakasangwe.
Diwani wa Kata hiyo anaitwa Joel Martin Mwakalebela.
HALI YA MIUNDOMBINU.
Kata ya wazo inayo miundombinu ya barabara za lami ambazo ni Barabara ya Bagamoyo, Mbuyuni na salasala.
Hali kadhalika inazo pia barabara za vumbi zinazotumiwa na wakazi wishio katika Mitaa yao.
HALI YA AFYA.
Hali ya Afya katika Kata ya wazo ni ya Kuridhisha, japokuwa wakazi wake mara kwa mara husumbuliwa na magonjwa ya MALARIA, PNEUMONIA, MAFUA NA UTI.
HALI YA ELIMU.
Hali ya Elimu katika Kata ya Wazo ni ya wastani.
SHULE ZA MSINGI ZA SERIKALI
Kata ya Wazo inazo shule tano za Msingi za Serikali ambazo ni :-
• Shule ya Msingi Salasala.
• Shule ya Msingi Benaco
• Shule ya Msingi Kisauke
• Shule ya Msingi Wazo
• Shule ya Msingi Nakasangwe.
SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI
Kadhalika Kata ya Wazo inazo pia shule tatu za Sekondari ambazo ni za Serikali kama ifuatavyo:-
• Shule ya Sekondari ya Twiga
• Shule ya Sekondari ya Kisauke
• Shule ya Sekondari ya Maendeleo.
MAHUSIANO YA WADAU.
Kata ya Wazo pamoja na wananchi wake inayo mahusiano ya kuridhisha na wadau wake , na ndio maana wanashirikiana kwa pamoja katika kusukuma maendeleo ya Kata yao.
MIRADI YA KUJIVUNIA KATIKA KATA.
• Ujenzi wa Kituo cha polisi ghorofa moja -Mtaa wa Madale kwa nguvu za wananchi.
• Ujenzi wa daraja la Mbopo.
• Uwepo wa maabara katika Sekondari zote tatu.
• Uwepo wa Zahanati tatu katika Kata.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz