• Malalamiko |
    • Anuani zetu |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Municipal Profile
  • Utawala
    • Idara
      • Human Resources
      • AFYA NA USAFISHAJI
      • Urban planning and Land Development
      • KILIMO NA MIFUGO
      • Secondary Education
      • Pre and Primary Education
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Community Development
    • Vitengo
      • sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Tehama
    • Kata
      • Kinondoni
      • Magomeni
      • Makumbusho
      • Mwananyamala
      • Kijitonyama
      • Wazo
      • Bunju
      • Mbezi juu
      • Ndugumbi
      • Msasani
      • Kawe
      • Mzimuni
      • Mabwepande
      • Tandale
      • Kigogo
      • Mikocheni
      • Hananasif
      • Kunduchi
      • Makongo
      • Mbweni
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Education
    • Afya
    • Maji naUsafishaji
    • entrepreneur and Soft Loan
    • Agricultural Consultancy
    • livestock keeping advice
    • Tax collection Centers
  • Madiwani
    • Baraza la madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyomalizika
  • Machapisho
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Miongozo
    • Fomu
    • Taarifa
    • Vipeperushi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya picha jongefu

Maji naUsafishaji

IDARA YA MAJI.

Idara ya Maji ni moja kati ya Idara zilizoko Katika Manispaa ya Kinondoni zenye majukumu yafuatayo:-

  • Kusanifu na kusimamia ujenzi na ukarabati wa Miradi ya Maji.
  • Kuunda vyombo vya watumiaji maji ili wananchi waweze kusimamia na kuendesha miradi yao ya maji katika ngazi ya jamii.
  • Kushirikiana na wadau mbalimbali ili kupata fedha na kutekeleza miradi mikubwa ya jamii ya kuwahudumia jamii.
  • Kutoa elimu kwa umma kwa njia mbalimbali juu ya hifadhi ya mazingira na uendeshaji wa huduma ya maji.
  • Kushirikiana na DAWASA, katika utekelezaji wa Mpango wa muda mrefu kuboresha vyanzo vya maji vilivyopo ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa vyanzo vipya vya maji.

TAARIFA YA HALI YA HUDUMA YA MAJI KATIKA MANISPAA YA KINONDONI

Huduma ya maji kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, kwa kiasi kikubwa hutolewa na Mamlaka ya Maji ya Mjini Dar es Salaam (DAWASA) ambayo imekodisha shughuli za utoaji huduma kwa kampuni ya DAWASCO. Malengo ya Kitaifa ni kuwapatia wakazi wa Mijini maji kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2015 na asilimia 100% ifikapo 2025.

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inakadiliwa kuwa na wakazi wapatao milioni 929,681ambao hupata maji kutoka katika vyanzo vya mto Ruvu, pamoja na maji chini ya ardhi. Maji yanayozalishwa yanakidhi mahitaji kwa asilimia 73. Upungufu wa maji unasababishwa na uwezo mdogo wa vyanzo vya maji vya miradi ya maji ambayo ilijengwa mwaka 1940 na 1976 wakati huo idadi wa wakazi wa jiji ilikuwa ni ndogo. Maeneo yasiyohudumiwa na Mtandao wa DAWASA hupata maji kutoka Miradi inayoendeshwa na Taasisi, Sekta binafsi na Jumuiya za watumia maji, chanzo kikubwa cha maji haya ni visima virefu. Katika Manispaa yetu ya Kinondoni kuna visima 97 vinavyomilikiwa na Manispaa. Aidha kuna visima vya taasisi na watu binafsi visivyopungua 300 katika maeneo mbalimbali ya Manispaa.

Pamoja na juhudi za DAWASA, kuna miradi ya maji inayotekelezwa na Halmashauri ya  Manispaa Kinondoni kupitia mapato yake ya ndani ambayo ni Madale Kisauke, Boko Chama, Makongo Juu, Magomeni Dosi, Magomeni Idrisa, Msasani Makangira, Ndugumbi, Kigogo Mbuyuni, Mzimuni na Bunju shule na kupitia wadau mbalimbali wa maji ikiwemo; Programu ya maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP)  Ujenzi wa mradi wa maji Mbuyuni Makongo ujenzi wake umekamilika, na visima vya Mbezi mtoni, Boko Dovya na Mabwepande  na Miradi ya Tandale uliofadhiliwa na shirika la Belgium technical Corporation.

HALI YA HUDUMA YA MAJI KATIKA MANISPAA YA KINONDONI

Halmashauri
Idadi ya visima
Idadi ya kamati
Idadi ya Jumuia
Idadi ya Wananchi 
Idadi ya wananchi wanaopata  huduma ya maji     
 
Binafsi
Serikali
 
 
 
 
Kinondoni
301
97
93
4
929,681
660,074


MAHITAJI YA MAJI KWA SIKU KATIKA MANISPAA YA KINONDONI.

NA
MAHITAJI YA MAJI KWA SIKU (L)
MAJI YANAYOPATIKANA KWA SIKU (L/DAY)

UPUNGUFU KWA SIKU (L)
1
              74,374,480.00
              54,293,370

              20,081,110

 

MIRADI ITAKAYOTEKELEZWA NA MANISPAA KATIKA MWAKA WA BAJETI 2016/17

NA
JINA LA MRADI
GHARAMA YA MRADI
CHANZO CHA FEDHA
1
Kumalizia mradi wa maji Makongo Mbuyuni
56,000,000.00
Mapato ya ndani
2
Kujenga kisima cha maji Mbopo
26,000,000.00
Mapato ya ndani
3
Kukarabati mradi wa maji Bustani ya Magomeni
25,000,000.00
Mapato ya ndani
4
Kufanya uchunguzi wa maji chini ya ardhi kuchimba na kuendeleza visima virefu viwili
60,000,000.00
CDG
5
Kuendeleza visima vya maji katika maeneo ya Mbopo, Kinondoni shamba, Mzimuni na changanyikeni
80,000,000.00
CDG
6
Kupanua mradi wa Maji Mabwepande mpaka Mbopo
55,280,000.00,  
World Bank

 

MIKAKATI YA  KUBORESHA HUDUMA YA MAJI KATIKA HALMASHAURI

  • Kuunda vyombo vya watumia maji ili wananchi waweze kusimamia na kuendesha miradi yao ya maji katika ngazi ya Jamii.
  • Kushirikiana na Wadau mbalimbali ili kuweza kupata fedha na kutekeleza Miradi mikubwa ya maji ya kuwahudumia jamii.
  • Kutoa elimu kwa umma kwa njia mbalimbali juu ya hifadhi ya mazingira na uendeshaji wa miradi ya Maji hususan ngazi ya Jamii.
  • Kushirikisha Sekta binafsi katika uendelezaji na uendeshaji wa huduma ya maji katika ngazi zote. 

MIRADI YA MAJI INAYOTEKELEZWA NA DAWASA 

Na
MRADI
MAELEZO YA MRADI
HATUA YA UTEKELEZAJI HADI 30/9/2016
GHARAMA YA MRADI
1
UPANUZI WA MTAMBO WA RUVU CHINI (MCC)
 
Kupanua mtambo kutoka uwezo wa sasa wa mita za ujazo 196,000kwa siku hadi mita za ujazo 270,000 kwa siku ili kukidhi mahitaji ya maji hadi mwaka 2032.
Upanuzi umekamilika na Mtambo sasa unazalisha lita milioni 270 kwa siku kuanzia tarehe 23/3/2016.
 
 
2
UKARABATI NA UPANUZI WA MFUMO WA KUSAMBAZA MAJISAFI
Mradi utatekelezwa kupitia mkopo kutoka Benki ya Exim India. Kazi hii inahusu miradi ya mabomba madogo na makubwa pamoja na kuunganisha wateja kwenye eneo kati ya Mbezi hadi Kiluvya na Tegeta hadi Bagamoyo. Jumla ya Km 511.6 za mabomba na Jumla  na matenki 4 yatajengwa katika maeneo ya Changanyikeni, Salasala, Wazo na Mabwe pande
 
Mkandarasi ameagiza asilimia 50 ya mabomba kutoka India, na amekamilisha upimaji wa njia za mabomba na mapitio ya usanifu wa mabomba na matenki, pamoja na mahitaji ya umeme wa pump za Booster Stations.
 
Dollar za Marekani milioni 32.927
3
UPANUZI WA MTAMBO WA RUVU JUU KUONGEZA UZALISHAJI MITA ZA UJAZO 114,000 KWA SIKU.
 Kupanua mtambo kutoka uwezo wa sasa wa mita za ujazo 82,000 kwa siku hadi mita za ujazo 196,000 kwa siku ili kukidhi mahitaji ya maji hadi mwaka 2032
Katika mradi huu mabomba mapya yamelazwa ili kubadilisha yaliyopo ambayo yamechakaa na ambayo ni madogo kuweza kusafirisha maji yatakayoongezeka. Mabomba yaliyolazwa ni kama ifuatavyo; bomba jipya lenye kipenyo cha 1200 mm, 40km kutoka Mlandizi hadi Kibamba na bomba la 1000mm, 10km kutoka Kibamba hadi Kimara, kuendeleza bomba la 900mm, 19.1 km kutoka Tanita hadi Kibamba, pamoja na ujenzi wa tanki moja lenye jumla ya mita za ujazo 10,000 eneo la Kibamba, Ujenzi wa mradi umefikia 97%
224,145,528,100.00
4
MIRADI YA KUBORESHA NA KUPANUA MFUMO WA UONDOSHAJI MAJITAKA
Mchakato wa kutafuta mkandarasi utaanza baada ya kukamilisha usanifu na kupata fedha.
DAWASA inaendelea na kutafuta maeneo kwa ajili ya ujenzi wa mitambo mipya ya kusafisha majitaka itakayojengwa Jangwani, Kurasini na Mbezi Beach.
 
Mchakato wa kumpata Mshauri atakayefanya mapitio ya usanifu na kutayarisha nyaraka za zabuni kwa ajili ya upanuzi wa mfumo wa majitaka umekamilika.
 

Matangazo

  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI TAREHE 14/08/2019. August 13, 2019
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI SIKU YA JUMATANO TAREHE 22/05/2019. May 20, 2019
  • TAARIFA KWA UMMA October 16, 2019
  • TANGAZO October 16, 2019
  • Tazama zote

Habari mpya

  • BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAPITISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    January 07, 2021
  • NI KINONDONI TENA UFAULU WA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020 MKOA WA DAR ES SALAAM

    December 24, 2020
  • NAIBU WAZIRI-OFISI YA WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA NAMNA KINONDONI INAVYOWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI

    December 22, 2020
  • HOSPITALI YA SANITAS YAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YA WATUMISHI WAKE

    December 22, 2020
  • Tazama zote

Picha Jongefu

TAMISEMI YAIPOGEZA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ilala Municipal website
  • Ubungo Municipal Council
  • Kigamboni Municipal
  • Temeke Municipal

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • eGoverment Agency
  • Manispaa ya Kinondoni yaongoza katika Makusanyo kufikia Dec.12,2017, 2017.
  • TUME YA UTUMISHI.Tangazo la nafasi za Kazi.

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Anuani zetu

    Dar es salaam, Tanzania

    Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road

    Namba za simu: +255 22 2170173

    Namba ya simu :

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Service

Hatimiliki