IDARA YA MIPANGOMIJI.
IDARA YA MIPANGOMIJI.
Idara ya Mipangomiji Manispaa ya Kinondoni imejumuisha vitengo vifuatavyo:-Mipangomiji, Uthamini, Ardhi, na Upimaji na Ramani na Mali Asili.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA MIPANGOMIJI.
Mipangomiji inayo majukumu mawili makubwa ambayo yamegawanyika kama ifuatavyo:-
•Kupanga (Planning and Design)
•Kusimamia Maendeleo ya ukuaji wa mji (Development control)
1.KUPANGA
•Kuandaa michoro ya Mipangomiji (town planning drawings) katika maeneo ambayo hayajaendelezwa kwa kiasi kikubwa.
•Kuandaa mipango ya urasimishaji makazi katika maeneo yaliyoendelezwa.
•Kuandaa mipango Kamambe (Masterplan)
2.KUSIMAMIA MAENDELEO YA UKUAJI WA MJI
•Kushughulikia maombi ya kumilikishwa ardhi kwa kutoa masharti ya uendelezaji katika majalada ya Hati.
Mahitaji ya kumilikishwa kiwanja ni:-
1.Kuwe na Mchoro wa Mipangomiji unaoainisha matumizi ya ardhi ya viwanja
2.Kiwanja kiwe kimepimwa na upimaji kuidhinishwa na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi
3.Mwombaji atachukua form za maombi ya kumilikishwa ardhi kutoka ofisi ya Afisa Ardhi wa Manispaa
4.Mwombaji atajaza form hizo atatakiwa kuziwasilisha zikiwa zimejazwa vizuri na aziambatanishe na Mchoro wa Mipangomiji na Ramani ya Upimaji wa kiwanja husika
Kushughulikia maombi ya vibali vya ujenzi
Mahitaji ya maombi ya vibali vya ujenzi:-
1.Mwombaji aandae michoro ya usanifu majengo (Architectural drawings) ya jengo analokusudia kujenga. NB: Kwa viwanja vyenye hati miliki, ujenzi unaokusudiwa uzingatie masharti ya uendelezaji yaliyoandikwa kwenye hati ya umiliki wa kiwanja
2.Kwa majengo ya ghorofa mwombaji atatakiwa kuandaa na kuwasilisha michoro ya vyuma ya jengo kusudiwa (structural drawings)
3.Mwombaji atatakiwa kuandika na kuwasilisha barua ya maombi yakibali cha ujenzi kwa Mkurugenzi wa Manispaa
4.Mwombaji atawasilisha michoro yake akiambatanisha na nakala ya hati miliki ya kiwanja katika ofisi ya Msanifu majengo wa Manispaa na atapatiwa form maalum za kujaza na baadae atafunguliwa jalada la maombi yake.
5.Kwa maeneo ambayo hayajapimwa (unplanned areas), mwombaji atatakiwa kupitia hatua na. 1-3 hapo juu.
6.Kujaza form mmalum ya maombi ya kibali cha ujenzi katika maeneo yasiyopimwa (form imeambatanishwa)
7.Kuwasilisha michoro ya majengo iliyoandaliwa ikiambatanishwa na form maalumu liyojazwa vizuri na Mchoro wa mipangpmiji wa eneo husika.
•Kushughulikia maombi ya mabadiliko ya matumizi ya Ardhi
1.Kuandika na kuwasilisha barua ya maombi ya kubadili matumizi ya Ardhi.
2.Barua iambanishwe na vitu vifuatavyo:-
a.Nakala ya hati/barua ya toleo.
b.Ramani ya michoro wa mipangomiji au (extract).
c.Ramani ya upimaji (kwa wale wenye offer pekee).
d.Nakala za risiti za malipo ya kodi ya ardhi.
e.Nakala za risiti za malipo ya kodi ya jengo kwa viwanja vilivyoendelezwa.
f.Michoro ya msanifu majengo (architectural drawings).
g.Nakala ya bango.
Mfano wa bango la tangazo la kusudio la kubadili matumizi ya ardhi limeambatanishwa.
Fomu ya kuomba kibali cha ujenzi wa maeneo yasiyopimwa fomu maeneo yasiyopimwa.pdf | Fomu ya kuomba kibali cha ujenzi wa maeneo yaliyopimwa
|
MFANO WA BANGO .pdf
|
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz