Kitengo cha ukaguzi wa ndani kimeanzishwa chini ya kifungu 45 (1) cha sheria ya fedha ya mamlaka ya Serikali za mitaa Na 13 ya mwaka 1982.
Kitengo hiki kinatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Kamati ya Ukaguzi.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI NI:-
1.Kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu za fedha za serikali zinafuatwa kama zilivyo ainishwa kwenye sheria mbalimbali za serikali.
2.Kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha zote za Halmashauri na kuandaa taarifa kwa Afisa Masuhuli.
3.Kufanya ufuatiliaji, ukaguzi na usimamizi wa fedha zote za Halmashauri zinakusanywa na Halmashauri kwa kutumia mifumo ya kieletroniki.
4.Kukagua na kutoa ushauri sahihi ili kuboresha utawala bora
5.Kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na mali za Halmashauri pamoja na kuhakiki uwepo wa thamani ya fedha.
6.Kuhakikisha malengo ya Halmashari yanafikiwa na kuwa na uwajibikaji.
7.•Kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu za fedha za serikali zinafuatwa kama zilivyo ainishwa kwenye sheria mbalimbali za serikali.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz