• Malalamiko |
    • Anuani zetu |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Municipal Profile
  • Utawala
    • Idara
      • Human Resources
      • AFYA NA USAFISHAJI
      • Urban planning and Land Development
      • KILIMO NA MIFUGO
      • Secondary Education
      • Pre and Primary Education
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Community Development
    • Vitengo
      • sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Tehama
    • Kata
      • Kinondoni
      • Magomeni
      • Makumbusho
      • Mwananyamala
      • Kijitonyama
      • Wazo
      • Bunju
      • Mbezi juu
      • Ndugumbi
      • Msasani
      • Kawe
      • Mzimuni
      • Mabwepande
      • Tandale
      • Kigogo
      • Mikocheni
      • Hananasif
      • Kunduchi
      • Makongo
      • Mbweni
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Education
    • Afya
    • Maji naUsafishaji
    • entrepreneur and Soft Loan
    • Agricultural Consultancy
    • livestock keeping advice
    • Tax collection Centers
  • Madiwani
    • Baraza la madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyomalizika
  • Machapisho
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Miongozo
    • Fomu
    • Taarifa
    • Vipeperushi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya picha jongefu

WAKAZI WA WAZO MJI MPYA WAPATIWA SULUHISHO LA BARABARA

Posted on: November 27th, 2020

Suluhisho hilo limekuja leo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo kuzuru eneo lenye bwawa na kushauri kufunguliwa kwa barabara ya muda katika mazungumzo yaliyohusisha  wananchi wa mji mpya, wamiliki wa viwanja vilivyopakana na bwawa pamoja na wadau wa maendeleo .

 Akizungumza na wakazi hao, Mhe. Chongolo amesema kufunguliwa kwa barabara ya muda kutawawezesha wakazi wa wazo mji mpya kufika majumbani kwao, lakini pia kutatoa nafasi ya eneo linalojaa maji kuboreshwa kwa kusambaza kifusi na kuchimba mitaro  itakayoelekeza  maji katika mkondo wake ili kuzuia athari za uharibifu wa barabara.

Amesema " Kwanza tuondoe hatari iliyo mbele yetu,  miti ing'olewe ili kuandaa eneo la barabara ya watu kupita ili waweze kufika katika makazi yao, kupatikane kifusi cha kujaza eneo kuyaelekeza maji kufuata mkondo wake, mana suala lililoko hapa ni makubaliano tu, baina ya mwenye kiwanja kilichopakana na bwawa kutoa eneo kwa muda ili waweze kusambaza kifusi kwa ajili ya kupata barabara ya muda, wakati tukiendelea kupata suluhisho la kudumu. jukumu langu ni kuhakikisha wananchi wanapata Amani katika makazi yao" Amesema Chongolo.

Aidha amemtaka Bw.Gerald Lusula Mwenye kiwanja Na.392 na Bwana Andrew Peter Mwenye kiwanja namba 393 vyote vikiwa vimepakana na eneo lenye bwawa kutoa ushirikiano katika kuhakikisha suluhu ya pamoja inapatikana kwa kuruhusu kusambazwa kifusi kwenye ukingo wa viwanja ili kupatikana kwa barabara ya muda kwa wakazi wa mji mpya kufika majumbani kwao huku wakiangalia suluhu ya kudumu ya eneo hilo.

Katika hatua nyingine ameiagiza  kampuni ya Mecco inayojenga barabara ya wazo kutumia scaveta pamoja na greda kusambaza kifusi kitakachotolewa na kiwanda cha wazo ikiwa ni pamoja na mifuko 20 ya cement pamoja na kalvati kwa ajili ya kuboreshwa eneo hilo la bwawa.

Awali akiainisha changamoto ya eneo hilo Mhandisi wa Tanroad Bi.Mariam Hassan amesema ni kutokana na kuzuiwa kwa mkondo huo wa maji hali iliyopelekea kutuama na kusababisha bwawa linaloendelea kukua na kuharibu barabara.


Imeandaliwa na

Kitengo Cha Uhusiano na Habari

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI TAREHE 14/08/2019. August 13, 2019
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI SIKU YA JUMATANO TAREHE 22/05/2019. May 20, 2019
  • TAARIFA KWA UMMA October 16, 2019
  • TANGAZO October 16, 2019
  • Tazama zote

Habari mpya

  • BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAPITISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    January 07, 2021
  • NI KINONDONI TENA UFAULU WA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020 MKOA WA DAR ES SALAAM

    December 24, 2020
  • NAIBU WAZIRI-OFISI YA WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA NAMNA KINONDONI INAVYOWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI

    December 22, 2020
  • HOSPITALI YA SANITAS YAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YA WATUMISHI WAKE

    December 22, 2020
  • Tazama zote

Picha Jongefu

TAMISEMI YAIPOGEZA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ilala Municipal website
  • Ubungo Municipal Council
  • Kigamboni Municipal
  • Temeke Municipal

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • eGoverment Agency
  • Manispaa ya Kinondoni yaongoza katika Makusanyo kufikia Dec.12,2017, 2017.
  • TUME YA UTUMISHI.Tangazo la nafasi za Kazi.

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Anuani zetu

    Dar es salaam, Tanzania

    Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road

    Namba za simu: +255 22 2170173

    Namba ya simu :

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Service

Hatimiliki