• Malalamiko |
    • Anuani zetu |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Municipal Profile
  • Utawala
    • Idara
      • Human Resources
      • AFYA NA USAFISHAJI
      • Urban planning and Land Development
      • KILIMO NA MIFUGO
      • Secondary Education
      • Pre and Primary Education
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Community Development
    • Vitengo
      • sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Tehama
    • Kata
      • Kinondoni
      • Magomeni
      • Makumbusho
      • Mwananyamala
      • Kijitonyama
      • Wazo
      • Bunju
      • Mbezi juu
      • Ndugumbi
      • Msasani
      • Kawe
      • Mzimuni
      • Mabwepande
      • Tandale
      • Kigogo
      • Mikocheni
      • Hananasif
      • Kunduchi
      • Makongo
      • Mbweni
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Education
    • Afya
    • Maji naUsafishaji
    • entrepreneur and Soft Loan
    • Agricultural Consultancy
    • livestock keeping advice
    • Tax collection Centers
  • Madiwani
    • Baraza la madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyomalizika
  • Machapisho
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Miongozo
    • Fomu
    • Taarifa
    • Vipeperushi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya picha jongefu

SIKU 36 ZA KINONDONI MPYA ZAZINDULIWA LEO

Posted on: July 23rd, 2018

NI KUFUATIA ZIARA YA DC -HAPI KATIKA KATA 20, ZA WILAYA YAKE, AKISIKILIZA, AKIKAGUA AKIJIRIDHISHA, AKISHAURI NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI WAKE KWENYE MKUTANO WA HADHARA.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ali Hapi amezindua operesheni ya siku 36, ya kusikiliza, kushauri na kutatua kero za wananchi katika Wilaya yake, ikiwa ni njia mojawapo ya kujiridhisha na utekelezaji wa utoaji  huduma sahihi kwa wananchi wake, kadhalika na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi unaozingatia sera, haki, wajibu,  viwango na usawa katika upatikanaji wa huduma hizo.

Operesheni hiyo imezinduliwa leo alipokuwa katika ziara yake hiyo na baadae kuzungumnza na wananchi wa Kata ya Tandale katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanjani hapo ambapo wakuu wa idara na vitengo, pamoja na taasisi mbalimbli zilitakiwa kutoa majibu ya kero hizo kwa wananchi.

Amesema azma yake kama Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, pamoja na Serikali inayotuongoza ni kuona, kuhakikisha na kujiridhisha na huduma zitolewazo kwa wananchi katika nyanja zote kwani ndio msingi imara uletao matokeo chanya katika kusukuma gurudumu la Maendeleo linaloenda sambasamba na uchumi wa viwanda kwa nchi yetu.

"Ni lazima sisi kama viongozi, tunaolipwa mishara kutokana na kodi zenu wananchi, tuhakikishe kazi zinafanyika, tujiridhishe wananchi wanasikilizwa, wanapatiwa huduma stahiki, na kero zinatatuliwa, watumikieni wananchi kwa wema, kwa upendo, kwa utii na kwa haki hiyo ndiyo ari ya Serikali ya awamu ya tano ya HAPA KAZI TU" Amesisitiza Hapi.

Alipokuwa akifafanua dhumuni hilo la operesheni yake amesema ziara hiyo itakuwa ni ya siku 36, ambapo kwa siku 20, atakuwa kila kata kukagua miradi, kusikiliza na kutatua kero, na kwa siku 16, ni kwa wakuu wa idara na vitengo wa Manispaa hiyo kuweka kambi katika Kanda 4 atakazozipanga kwa lengo la kuhakikisha kero, na maelekezo yanafanyiwa kazi.

Alipokuwa akifafanua utekelezaji wa ilani ya CCM,  kwa Wilaya yake, Mkuu huyo amesema, kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Wilaya yake ilitenga bilioni 3.8,kwa ajili ya mikopo ya wanawake na vijana, ambapo hadi sasa zimetumika tsh bilion 1.9, ambayo ni sawa na asilimia 50%, imesikiliza kero za ardhi zisizopungua 637, pamoja na kutengeneza madawati yasiyopungua 7 , 319.ili kuhakikisha wanafunzi wanapatiwa huduma bora za elimu.

Kadhalika akijibu kero za ardhi zinazoshughulikiwa na mabaraza ya Kata Hapi alifafanua kuwa mabaraza ya Kata,  hayapaswi kisheria kusikiliza shauri linalozidi thamani ya tsh milioni tatu,   na kwa upande wa kero ihusuyo upungufu wa madawa kwenye zahanati na vituo vya Afya amemtaka Mganga Mkuu wa Manispaa ndg Festo Dugange kutoa elimu  kwa wananchi ya zipi dawa zinapatikana katika vituo vya Afya na Zahanati hizo

Hii ni safari ya mafanikio kuelekea siku 26, za kuwatumikia wananchi kwa ukaribu zaidi, ambapo ameanzia katika Kata ya Tandale  na baadae kuongea na wanachi kwenye mkutano wa hadhara ambapo kero mbalimbali zihusuzo afya, mazingira, miundombinu, maswala ya vyeti vya kuzaliwa,maswala ya elimu zimetatuliwa.


Imeandaliwa na

Ofisi ya Uhusiano na habari.

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI TAREHE 14/08/2019. August 13, 2019
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI SIKU YA JUMATANO TAREHE 22/05/2019. May 20, 2019
  • TAARIFA KWA UMMA October 16, 2019
  • TANGAZO October 16, 2019
  • Tazama zote

Habari mpya

  • BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAPITISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    January 07, 2021
  • NI KINONDONI TENA UFAULU WA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020 MKOA WA DAR ES SALAAM

    December 24, 2020
  • NAIBU WAZIRI-OFISI YA WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA NAMNA KINONDONI INAVYOWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI

    December 22, 2020
  • HOSPITALI YA SANITAS YAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YA WATUMISHI WAKE

    December 22, 2020
  • Tazama zote

Picha Jongefu

TAMISEMI YAIPOGEZA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ilala Municipal website
  • Ubungo Municipal Council
  • Kigamboni Municipal
  • Temeke Municipal

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • eGoverment Agency
  • Manispaa ya Kinondoni yaongoza katika Makusanyo kufikia Dec.12,2017, 2017.
  • TUME YA UTUMISHI.Tangazo la nafasi za Kazi.

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Anuani zetu

    Dar es salaam, Tanzania

    Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road

    Namba za simu: +255 22 2170173

    Namba ya simu :

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Service

Hatimiliki