KATA YA MZIMUNI
Kata ya Mzimuni kwa asili ya jina lake ni kutokana na Chemchem ya maji iliyokuwepo eneo hilo, ambapo ilikuwa ikifika saa 6:00 mchana inasadikiwa kuwepo na harakati za watu wasioonekana wakisikika kufanya shughuli zote za kibinadamu.
Chemchem hiyo kwa wakati huo ilikuwa katika mpaka wa Mtambani na Mwinyimkuu , kwa sasa kutokana na mji kukua na watu kujenga na shughuli kuongezeka imekuwa sio rahisi tena kusikia watu au kitu chochote kisicho katika mazingira ya kusadikika kikiendelea katika eneo hilo.
IDADI YA MITAA.
Kata ya Mzimuni imeundwa na Mitaa minne ambayo ni
1. Mtaa wa Makumbusho
2. Mtaa wa Mwinyimkuu
3. Mtaa wa Idrissa
4. Mtaa wa Mtambani.
Diwani waKata hiyo ni Ally Kondo.
MAENDELEO YA KATA.
HALI YA ELIMU
Hali ya elimu Katika Kata ni ya kuridhisha.
HALI YA AFYA.
Hali ya Afya Katika Kata pia ni ya kuridhisha.
HALI YA MIUNDOMBINU.
Kata ya Mzimuni inayo miundombinu ya barabara ya lami pamoja na vumbi.
MAHUSIANO NA WADAU.
Wananchi wa Kata ya Mzimuni wanashirikiana bega kwa bega na wadau wao katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana .
MIRADI WANAYOJIVUNIA KATIKA KATA.
Mradi wa Malaria pamoja na mradi wa MDH.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz