KADI YA MSAMAHA WA MATIBABU MANISPAA YA KINONDONI.
Kadi ya Msamaha wa Matibabu hutolewa kwa wazee kuanzia umri wa Miaka 60.
Mzee huyu lazima awe Mkazi wa Manispaa ya Kinondoni.
Kadi hii hutolewa bure, hakuna malipo yeyote.
UTARATIBU WA KUPATA KADI YA MSAMAHA.
• Muhusika anatakiwa kupata barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa wake anakoishi.
• Barua hiyo ya utambulisho iambatishwe na Picha ya pass port moja.
• Baada ya kukamilisha taratibu hiyo, Muhusika afike ofisiza Mganga Mkuu wa Manispaa zilizopo Mkabala na Kituo cha Afya cha Magomeni(Barabara ya Kawawa na Morogoro), kwa ajili ya kupiga Picha itakayotumika kwenye Kadi yako , pamoja na kupewa taratibu nyingine na tarehe ya kuchukua kadi yako .
KADI YA MSAMAHA INATUMIWAJE
Kadi hii hutumika kwenye vituo vya Afya, Zahanati pamoja na hospital zilizopo Manispaa ya Kinondoni.
Mtumiaji atatakiwa kufuata taratibu zifuatazo pindi atakapokuwa na uhitaji wa kupata matibabu.
Kwanza anatakiwa kuanzia Zahanatiiliyopo karibu nae kwa ajili ya kupata huduma,itakapoonekana kunauhitaji wa uangalizi mwingine na matibabu mengine Muhusika atatakiwa kupewa barua ili aweze kwenda Kituo cha AFya kwa matibabu.
Kadi hii itatumika kwenye Hospital ya Mwananyamala endapo tu huduma anazotakiwa kuzipata mgonjwa zimeshindikana kwenye Zahanati na vituo vya Afya, na Mgonjwa huyu atatakiwa kupewa barua ya kumuelekeza kwenda hospital hiyo yaani(Referral letter).kwa ajili ya matibabu zaidi.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz